Rais Samia afunga mjadala wa machinga; ataka wapangwe vyema bila uonevu


Mkuu heading yako inasema mkuu wa nchi kafunga mjadala halafu ww mwenyewe tena umefungua bandiko khs machinga huoni kama unapingana na mkuu wa nchi kitu ambacho ni hatari kwako?
 
Asili ya biashara ya umachinga ni kuzurura, kuzagaa na kusongamana. Kamwe mmachinga hawezi kukaa sehemu moja, kupangika na kukwepa msongamano.

Dawa ya wamachinga sio kuwapatia eneo lao rasmi la kukaa na kuwapangwa, dawa ni kupiga marufuku biashara holela.
 
Niliwaambia urafiki kati ya CCM na wamachinga hauwezi kuisha, kwa kauli hii hamna mmachinga anabakia kuwa mtu asiyegusika.
 
Dawa ya tatizo la machinga ni "Rural Economic Development". La sivyo uchafuzi wa miji utaendelea pamoja na kutengeneza bomu litakalolipua jamii.
 
Rais ana lugha lainiiiiii. Sijui nilivyomwelewa nipo sahihi?

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Ila mbona makusanyo yameongezeka? Mwezi uliopita makusanyo yalikuwa trillion 1.6.

Kipindi Cha kikwete ambapo machinga hao unaowasema hawakuwepo lakini makusanyo kwa mwezi ilikuwa bil 800
Unadhani makusanyo ya tra yanategemea maduka tu,pole
 
hawajajengewa "kiburi" ila LIJIBURI, mfumo wa CCM umekuwa hovyo kabisa unaharibu hii nchi, eti watafutiwe utaratibu, kwani haifahamiki utaratibu ni kuuza bidhaa madukani au sokoni?
kwahiyo kesho watu wakianza kunya barabarani mtawaambia wakae watafutiwe utaratibu wa kujisaidia?
 
Sisi machinga ni wapiga kura, tunatoa rai... mtuguse tunuke🐒
Hivi bado tu unaamini kwamba ccm ya leo inajali unapigaje kura? Hiyo ilikuwa kabla ya Magufuli bwashee. Watu wanaandaa kura zao na kuzihesabu na ndio zinazotangazwa. Sasa wewe endelea kujivunia kakura kako
 
Wafanyabiashara wanalipa kodi nyingi sana lakini wanapokaguliwa huwa hawabembelezwi kama ifanyikavyo kwa wamachinga, ninadhani kuna siri kubwa tusiyoijua kati ya viongozi na wamachinga. Inawezekana viongozi wanafanya biashara kubwa kupitia wamachinga kwani baadhi ya wamachinga bidhaa zao ni zaidi ya maduka.
 
Siri kubwa ni CCM imetengeneza kizazi cha mambumbumbu ambao wanatumika kipindi cha uchaguzi tu, kwa maslahi yao.
Hakuna waziri anayekwenda kununua nyanya zilizopangwa juu ya kinyesi pale Kariakoo, wao wananunua mlimani city na City Mall, hawa watu ni hatari sana.
 
Hivi nchi za wenzetu hawanaga wamachinga? Kwa mliobahatika kutoka nje ya nchi hii naomba mnisaidie mie mwenzenu au nao bado wanakimbizana nao kama huku?
 
CCM huwa haitegemei kura ya mtu kwani yenyewe hutoa uamuzi CCM ishinde kwa vyovyote vile. Wananchi hupoteza muda wetu kwenda kupiga kura wakati tayari CCM imekwisha amua ushindi, wakati wa kupiga kura wamachinga wao wako kwenye biashara zao na wengi wao hawana vitambulisho vya mpiga kura, CCM inawatumia kuhalalisha wizi wa ushindi.
 
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu.

Hiyo ni Go ahead ya Wamachinga kuondolewa. Hiyo kinga hakuna tena ya kutoguswa.
Mkuu watu hawaelewi kwa sababu kabla hata mtu hajasema neno wao wameshaelewa tayari
 
Mkuu watu hawaelewi kwa sababu kabla hata mtu hajasema neno wao wameshaelewa tayari
Hauwezi kumbembeleza mmachinga na akaondoka hapo alipo hata angekuwa mwanao hawezi kukubali. Mwaka huu utakwisha na wamachinga watakuwa barabarani kama walivyo. Ni vipi nyie hamjui kuwa wamachinga hujengewa maeneo mazuri ya kufanyia biashara lakini huyatelekeza.
 
sawa na wale ndege wanaokaa migongoni mwa wanyama mbugani
Mhhh hawa ndege unawaonea....wale ndege wala sio wasumbufuy kwa wale wanyama...ki ukweli wote pale wanafaidika mmnyama anawapa hidhafi na ndege wanamsaidia mnyama kuondoa wadudu wasumbufu...sasa sijajua muktadha wako wa kufananisha "machinga" na hao ndege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…