Rais Samia afunga mjadala wa machinga; ataka wapangwe vyema bila uonevu

Kikubwa serikali ifungue milango ya ajira hao Machinga wengi ni wasomi wa Diploma + Degree kutokana na changamoto ya ajira ndio wamekimbilia huko
 
Ninazijua faida za ndege rafiki kwa wanyama, mfano wangu ni jinsi wamachinga wanavyopishana na vijiko vya ujenzi wa barabara bila kujali hatari iliyopo, wajenzi wanalazimika kuepusha ajali na kuzikwepa bidhaa zilizopangwa eneo la ujenzi.
 
Unaahisi wamachinga wataondoka bila kelele na vurugu? Ukisema uwapange vizuri, kwa jiji Kama la dar utawapeleka wapi?
Kikwete alijenga machinga complex Ila bado hawakwenda
Sio kama hawakwenda vile vizimba walipeana wakubwa watupu ambao sio machinga! Then machinga halisi walikosa karibu wote!
 


Ni vigumu sana wavunja sheria haohao wakafuata sheria
 
Sio kama hawakwenda vile vizimba walipeana wakubwa watupu ambao sio machinga! Then machinga halisi walikosa karibu wote!
Mbona hivi karibuni walipewa na wakaondoka, tatizo lao kila mmoja anataka awe mbele ya mwenzake na ukiwapa ghorofa wote wanataka wakae chini na hapo chini kila mmoja anataka awe mbele!
 

Haya maneno hayatatui chochote
 
Kupangwa vizuri ndio kuwapanga vipi.
Kauli za mtu dhaifu, wapangwe vizuri ndio nini wakae mstari kama shule au? Kiongozi asiyekuwa dhaifu atasema sheria zipo na lazima zifuatwe bila kutumia nguvu ila inapokuja watu wanapinga sheria nguvu itatumika japo hatutaki kufika huko. Lakini unawapa kazi wakuu wa mikoa wafanya halafu huwapi tools au backup ili wakiharibu useme sikusema ni dalili za udhaifu. Kiongozi wakati mwingine unafanya maamuzi magumu ila yenye tija. Unasema hawalipi kodi, inafanya uchochoro wa wenye maduka kuwatumia, unasema tukusanye kodi halafu unasema wapangeni vizuri. Hivi wapangwe au wasifanye biashara sehemu zisizoruhusiwa? kazi tunayo.
 
Unalinganisha billion 800 ya mwaka 2012 ?

Na kuilinganisha na uchumi wa Sasa

Angalia Kwanza exchange ya dollar kipindi kile na sasa
Walichofanya kupora na zile kodi za halmashauri zamani na zote kulipwa serikali kuu baade ndio wanagaiwa ndio maana mfuko kama umetuna kidogo lakini kama ulivyosema 800 ya wakati ule sio ya leo.
 
Unataka afokefoke?? Mama anaongea kwa matendo na kalamu zaidi
Kama anaongea na kalamu aache hii kauli kila siku msidhani mimi dhaifu, huko ni kujishuku mwenyewe nani huyo aliyesema yeye dhaifu.
 
Raisi anaongea vitu visivotekelezeka..machinga huwezi kumtoa bila nguvu coz huwa hawakubali kutoka wenyewe kwa amani pili machinga huwa hawako interested na maeneo wanayopangiwa maana pale alipo kwake ndio sehemu sahihi kwake na sio pengine.Hao Ni nguvu mwanzo mwisho..wafanye Kama walivofanya ubungo mataa ,waliwapa deadline..usiku wa manene jiji ikaondoa vibanda vyote..Asubuhi wanakuta peupe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kikubwa serikali ifungue milango ya ajira hao Machinga wengi ni wasomi wa Diploma + Degree kutokana na changamoto ya ajira ndio wamekimbilia huko
Kama tumefikia kusema wamachinga ndio kimbilio la wasiokuwa na kazi basi huko mbeleni ni majanga makubwa sababu number ita double miaka inayokuja. Wamachinga hawachangii pato la taifa sanasana wanaharibu mazingira na kichaka cha kukwepa kodi wenye maduka. Huwezi kusema dukani lazima risiti hapo nje kakaa na vitu hivyohivyo kapewa na mwenye duka anauza bila risiti huu ni ujinga uliopitiliza. Mwenye duka utakuta hana wasiwasi kakaa tu utasema hauzi lakini mbele kaweka wamachinga wake hana shida. Hakuna nchi duniani ikaendelea kwa wamachinga lazima maamuzi magumu yafanyike.
 
Mama mwenyewe anasema anaenda kuchapa kazi ya marekebisho, sasa unategeme upande wa machinga kutakuwa na mabadiliko!.
 
Machinga yuko mbele ya duka halipi kodi, mwenye duka analipa Jiji kodi ya maendeleo kwa ajili ya usafi huku anayechafua halipi!
 
Inawezekana akili ikitumika. Kwa maeneo yenye mzunguko mkubwa Kila kituo cha machinga anapoweka bidhaa kirasimishwe na alipe post tax kulingana na mauzo bila kujali mzigo ametoa wapi, kodi iwe attached na tin na tin iwe attached na post, post ziwe na camera review, one camera 10 post kulingana na angle, wapewe bure efd's na kufundishwa kutoa risiti. Hapa wengi wataogopa kuchukua mzigo wa wenye maduka maana wakichukua watalipa kodi kwa niaba na wakikaa na mizigo yao watalipa kodi kuwepo kwenye post. Akitaka kukwepa aende eneo la machinga lisilo na mfumo rasmi wa post tax.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…