Rais Samia afunga mjadala wa machinga; ataka wapangwe vyema bila uonevu

UDUANZI huu...
Machinga ni lazima akae kwenye maduka ya watu??

Wamewaacha wamekaa mpaka wanaona yale maeneo wanayamiliki serikali ya CCM bana, tuwapelekee hawa wamachinga wakajenge vibanda vyao Masaki na Oysterbay kule SeaCliff.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
U
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu.

Hiyo ni Go ahead ya Wamachinga kuondolewa. Hiyo kinga hakuna tena ya kutoguswa.
Una mawazo kama yangu hakika upo sahihi ni muda wa machinga kutolewa barabarani kimya kimya bila kelele.
 
Hujamuelewa Mh Rais.

Kasema waondolewe kwa utaratibu bila kelele na vurugu.

Hiyo ni Go ahead ya Wamachinga kuondolewa. Hiyo kinga hakuna tena ya kutoguswa.
Mtanzania umuondoe kwa utaratibu? ...kesho yake tu atarud na anajua la kumfanya huna
 
Maajabu niliyakuta stendi ya sabasaba Dodoma, bidhaa wanaweka chini mabasi yanafanya kukwepa mmchinga aliyeweka bidhaa chini
Iko hivyo hata huku Arusha.

Kuna siku nimezenguana na Mama mboga, wakati napisha Gari nikagonga Nyanya zake alizopanga chini zikaporomoka...si akaanza kunikoromea sikumnyamazia, tukapambana pale sema tu nikamstahi kama Mama nikaamua kuishia zangu.

Yaani kwa akili zake alitaka mimi nisuguane na gari alafu nithamini nyanya zake....sijui huwa akili wanapelekaga wapi haw Watu.
 
Hakuna chochote hapo majinga hawezi kupanga kwa njia hiyo
 
Samia anawaonfoa wamachinga kwa staha na ustaarabu,na ujue anaposema wakuu wa mikia na wilaya wawapange ujue tayari kila kitu kimepangwa na kinafuata ni utekelezaji tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Aah hakuna kitu kama hicho.machinga hata kwa kutumia tu nguvu ni ngumu kuwaondoa.
Wiki iliyopita Amos Makalla alienda pale kariakoo akawaambia mwisho kukaa barabarani ni wiki hii jumatatu
Ila leo ni ijumaa hakuna hata mmoja aliyeondoka
 
Aah hakuna kitu kama hicho.machinga hata kwa kutumia tu nguvu ni ngumu kuwaondoa.
Wiki iliyopita Amos Makalla alienda pale kariakoo akawaambia mwisho kukaa barabarani ni wiki hii jumatatu
Ila leo ni ijumaa hakuna hata mmoja aliyeondoka
Amewapa mwezi mmoja wawe wameondoka! Ndani ya huu mwezi mmoja anajua tutakuwa tumesahau.
 
Ndiyo madhara ya wanasiasa kutunga Sera mbovu ili wafanye siasa tena Sera za majukwaani 'uncertainty policies'
 
Aah hakuna kitu kama hicho.machinga hata kwa kutumia tu nguvu ni ngumu kuwaondoa.
Wiki iliyopita Amos Makalla alienda pale kariakoo akawaambia mwisho kukaa barabarani ni wiki hii jumatatu
Ila leo ni ijumaa hakuna hata mmoja aliyeondoka
Tuna Sera mbovu sana pita kuanzia saa 12 jioni nje ya maduka tunauza chips barabarani ,kwenye maduka yetu mchana kweupe tunapanga bidhaa hadi barabarani na kuziba maduka mengine serikali iko kimya ,watawala wanapokaribia na uchguzi mkuu wanaruhusu haya yote hakuna utaratibu
 
Mamlaka ya kukomba kura zote wanayo lakini bado hawajiamini kutokana na chama kuwa dhaifu siyo kama walichoachiwa na Nyerere.
 
Huku tukiendelea na mjadala, tangu lini serikali inawahamisha wanaovamia maeneo kwa sala ya bwana! Au baada ya kuning'izwa mtu kama popo!
Wamachinga waondoke tu.
 
Habari hii hapa kutoka kwa Msemaji mkuu wa serikali, ukibisha nakuletea na video
View attachment 1936895
Hauwezi kujenga nchi kwa kununua ndege na kuzifuga, ndege hizo huwa hazifugiki kwakua hazitagi. Mambo mengi ambayo yangefanyika baada ya uhuru mpaka leo bado hayajafanyika, Dar bado nyumba nyingi hazina maji kwa sababu huduma ya maji bado duni! Tumejikita zaidi kusubiri uchaguzi ili tuporane kura kuliko kuijenga nchi. Vijana kukimbilia mijini kunatokana na serikali kutokuwa na mipango yoyote ya maendeleo vijijini zaidi ya kufanya mikutano ya propaganda, miaka kumina tano iliyopita tuliambiwa vijijini kuna maji lakini kila siku wananchi wanalalamika hakuna maji. Mkoloni aliweka vyuo vya maendeleo vijijini sisi tunaweka Veta mijini! Manerumango kuna miundombinu ya kukiendeleza chuo cha maendeleo lakini badala yake CCM inaendeleza matawi ya chama! Matokeo yake vijana wanakimbilia mijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…