Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakuu,
Rais Samia ashiriki halfa ya Utoaji Tuzo kwa Walipakodi wa Bora kwa Mwaka 2023/2024 leo Januari 23, 2025.
RAIS SAMIA
Rais Samia ameongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuzipa tuzo hizo hadhi kubwa zaidi na kuhakikisha zinapata uzito unaostahili katika kutambua na kuenzi mafanikio ya wahusika.
Pia Rais Samia alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanapohitajika kulipa kodi hudai kuwa kuna maelekezo kutoka juu.
Hata hivyo, Rais Samia amesisitiza kwamba katika serikali ya Tanzania, uongozi wa juu ni nafasi ya Rais, na kwa kuwa yeye ndiye Rais, ameeleza wazi kuwa hajawahi kutoa maagizo yoyote kwa mtu yeyote ya kutolipa kodi.
ALBERT CHALAMILA
Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila alimpongeza Rais Samia kwa kupitshwa kama mgombea wa CCM kwenye Uchaguzi mkuu ujao.
Chalamila pia alidokeza kwamba uongozi wa jiji la Dar Es Salaam umejipanga kuanza kutengeneza mazingira ya wafanyabiashara kufanya kazi masaa 24 lengo likiwa ni kuongeza wigo wa ajira kwa vijana na kupanua huduma kwa wananchi.
Chalamila amesema uongozi wake uko mbioni kuweka taa za usiku pamoja na CCTV camera, ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya kazi usiku
PAUL MAKANZA
Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Paul Makanza alipongeza serikali kwa kuishirikisha TPSFkwenye kutoa maoni kwenye mchakato wa dira ya Taifa ya kuelekea 2050 ambapo Makanza alisema kuwa kushirikishwa kwenye mchakato huo ni kuthamini mchango wa sekta binafsi nchini
STEVEN LUSINDE
Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania alimpongeza Rais kwa kuwapatia wamachinga fedha za kuendesha shughuli zao na aliongeza kwa kusema kuwa kwa niaba ya Wamachinga, anamuunga mkono Rias Samia kwenye Uchaguzi wa 2025
Rais Samia ashiriki halfa ya Utoaji Tuzo kwa Walipakodi wa Bora kwa Mwaka 2023/2024 leo Januari 23, 2025.
RAIS SAMIA
Akizungumza leo katika hafla ya utoaji wa tuzo, Rais Samia ametangaza kwamba kuanzia mwaka ujao, tuzo hizo hazitasimamiwa tena na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bali zitakuwa chini ya Ofisi ya Rais.Rais Samia ameongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuzipa tuzo hizo hadhi kubwa zaidi na kuhakikisha zinapata uzito unaostahili katika kutambua na kuenzi mafanikio ya wahusika.