Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia mgeni rasmi katika kilele cha Miaka 10 ya ujenzi wa Female Future Program chini ya Waajiri (ATE)
Karibu kufuatilia kinachojiri
Akizungumzia Female Future Program chini ya Waajiri (ATE)
"Niushukuru uongozi wa chama cha waajiri TANZANIAATE kwa kunialika kushiriki maadhimisho haya ya progam hii inayolenga kuongeza ujuzi kwa wanawake viongozi lakini kubwa zaidi niwashukuru waanzilishi wa program hii, na leo ni faraja yetu kwamba programu hii inaendelea vizuri sana. Nikikumbuka nilipokuwa mgeni rasmi wakati programu hii inapoanza inanipa faraja sana kuona kuwa leo miaka kumi baadaye program hii imegusa maisha ya wanawake wengi."
"Tangu program hii ianze mwaka 2015 imeshanufaisha wanawake 462, sekta binafsi na sekta ya umma ambapo kati ya hao wanawake 16 wameshafika ngazi ya watendaji wakuu katika makampuni mbalimbali, aidha wanufaika wa program hii 56 tayari ni wajumbe wwa bodi mbalimbali katika sekta za umma."
Akitoa pongezi na ujumbe kwa wahitimu awamu ya 10 wa program hiyo.
"Ninyi mna dhima kubwa ya kuwasaidia wanawake wenzenu, hapa simaanishi kwamba mkawapendelee bali mkawaongoze muwasaidie wanyanyuke, mna kila sababu ya kufanya hivyo ninyi mnajua machungu na hila za mlikotoka kwa wanawake, sasa mkiwasaidia mtakuwa wengi zaidi nafasi za juu na mtaweza kusukuma ajenda zenu kwa uzuri zaidi."
"Nendeni mkawe chachu ya maendeleo katika jamii elimu mnayopata na stadi za uongozi mnazopewa zikainufaishe jamii, familia na taifa kwa ujumla haitegemewi kuwa usomi au nafasi ya kiuongozi unayoipata mwanamke iwe sababu ya kuvuruga familia au kuharibu watoto wake, mna dhima kubwa ya kuendelea kuhakikisha jamii inaendelea kuwa na imani na amani katika maeneo tunayoishi, elimu na nafasi za uongozi zisitufanye tukasahau wajibu wetu wakijamii wa malezi na makuzi ya watoto wetu"
Akizungumza kuelekea uchaguzi
"Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, ni mwaka wa kuikataa kwa vitendo ile kasumba na dhana, hapa nazungumza na wabunge na wengine mliohitimu na mtapenda kuingia nafasi za siasa. Ni mwaka wa kuikataa ile dhana potofu kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke, adui wa mwanamke si mwanamke, adui wa mwanamke ni mila potofu na uduni wa uchumi wetu na mengine kama hayo."
"Wanufaika wa female future program ikiwemo wabunge mkawe mstari wa mbele kutumia fursa hii kuongeza idadi ya wanawake wenye sifa na uwezo kwenye vyombo vya maamuzi, fanyeni hivyo kwa nyinyi wenyewe kujitokeza kama wagombea majimboni au kwa kuhamasisha wanawake wenye sifa, uwezo na wito wa kiuongozi kuijitokeza kwenye nafasi hizo na kuunga mkono kwa kuwapigia kura nyingi."
"Nawapa shime wanawake jitokezeni kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa mwaka huu lakini pia hakikisheni mnajiandikisha na kurekebisha taarifa zenu kwenye daftari la wapiga kura kwa sababu ukiwepo pale ndio unaweza kupiga kura."
View: https://www.youtube.com/live/BQDpwewcZEw?si=p-m4IIiPzf-aTdwq

Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025