Rais Samia akagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli, ujenzi wafikia 93%

Rais Samia akagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli, ujenzi wafikia 93%

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
IMG-20241013-WA0103.jpg

Muonekano wa Daraja la JP. Magufuli linalounganisha eneo la Kigongo (Misungwi) na Busisi (Sengerema) lenye urefu wa KM 3 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66. Mkoani Mwanza, Oktoba 13, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66, linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita kupita Ziwa Victoria ambao umefikia asilimia 93, leo Oktoba 13, 2024 Mkoani Mwanza.

IMG-20241013-WA0092.jpg

IMG-20241013-WA0100.jpg
Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa shilingi Bilioni 716.3 zikijumuisha Malipo ya Mkandarasi, Mhandisi Mshauri wa usimamizi wa mradi, Fidia na Usanifu.

Akitoa taarifa ya mradi, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa wakati ili ujenzi wa daraja hilo uweze kukamilika na kutumika ifikapo mwezi Februari, 2025.

Bashungwa ameeleza kuwa Mkandarasi amekamilisha kumwaga zege kwenye daraja lote na anaendelea na ujenzi wa barabara za maungio kilometa 1.66 kwa kiwango cha lami pamoja na kuweka mazingira ya daraja safi kwa kujenga kingo na kuweka alama za usalama.

Mradi wa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli unasimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) chini ya Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation akishirikiana na China Railway 15 Bureau Group Corporation (CCECC - CR15G JV) na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri kampuni ya Yooshin Engineering Corporation (Korea) akishirikiana na Cheil Engineering Co. Ltd (Korea), Rina Consulting S.P.A (Italia) na Afrisa Consulting Ltd (Tanzania).
WhatsApp Image 2024-10-13 at 19.54.23_4e2ce3fc.jpg

WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.48.49_b83c21a8.jpg

Soma Pia:
~ Ujenzi wa Daraja la Magufuli wafikia Asilimia 90

~ Bashungwa: Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli Mbioni Kukamilika, Bado Mita 2 Daraja Kuunganishwa
~ Injinia: Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi umefikia 88.61%, litaanza kutumia Desemba 30, 2024
~ Ujenzi wa Daraja la J.P.Magufuli (Kigongo - Busisi) Wafikia 85%
 
Bwana ee

IMG_0467.jpeg

Mkimaliza Mseme

IMG_0468.jpeg

Mnamsumbua mama

IMG_0464.jpeg

Na hesabu zenu
IMG_0465.jpeg

Za Asilimia

IMG_0469.jpeg
 
Safari ya masaa mawili sasa kwa dakika 4 tu.

Uzuri wa teknolojia.
 
Mradi wa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli unasimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) chini ya Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation akishirikiana na China Railway 15 Bureau Group Corporation (CCECC - CR15G JV) na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri kampuni ya Yooshin Engineering Corporation (Korea) akishirikiana na Cheil Engineering Co. Ltd (Korea), Rina Consulting S.P.A (Italia) na Afrisa Consulting Ltd (Tanzania).
Wachina wamekwama wapi mpaka wamchukue Korea
 
Back
Top Bottom