Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia Hassan Suluhu ndiye mgeni rasmi wa kikao kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, leo Jumanne Juni 18, 2024.
SUNGURA: KATI YA WANAHABARI 20,000 NCHINI, NI 4,000 TU NDIO WANA MIKATABA
Ernest Sungura ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (#CoRI) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (#MCT) amesema kilio kikubwa cha Wanahabari ni kufanya kazi bila Mikataba, bila Mishahara na wachache wenye Mishahara hawapati kwa wakati.
Amesema “Utafiti wa Umoja wa Klabu za Wandishi wa Habari (UTPC) unaonesha Asilimia 80 ya Waandishi wa Habari hawana Mikataba, pia takwimu za Idara ya Habari MAELEZO na TCRA Vyombo vy Habari vilivyosajiliwa ikiwemo Magazeti, Redio, TV na Mitandao vinafikia 1,000.”
Ameongeza “Makisio yanaonesha, kati ya Waandishi na Wafanyakazi wa Habari katika Vyombo vilivyosajiliwa ni 20,000, kati yao ni 4,000 ndio wenye Mikataba, wengine 16,000 waliosalia hawana Mikataba.”
ERNEST SUNGURA: TBC ITUMIKE NA WANASIASA KWA USAWA
Ernest Sungura ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) amesema Kitu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linatakiwa kutoa haki sawa kwa Wanasiasa wote hasa wakati huu ambapo Nchi inaelekea kwenye Uchaguzi.
Amesema “Sisi CoRI tunashauri haki sawa kwa wanasiasa wote wa vyama vyote katika kuvitumia vyombo vya habari hususan chombo cha Umma cha Utangazaji kama TBC.”
TIDO MHANDO: VYOMBO VYA HABARI VINA MAUDHUI MEPESI VINAACHA TAARIFA ZA UWAJIBIKAJI
Mwanahabari Mkongwe, Tido Mhando amesema mazingira magumu ya Kisheria na Kisiasa Nchini yamechangia Vyombo vya Habari kutawaliwa na taarifa au maudhui ya Burudani, Mapenzi, Muziki, Michezo, Filamu na mengine yenye tija ndogo kutokana na wasiwasi uliopo kwa Waandishi wa Habari.
Ameyasema hayo wakati akiwasilisha Ripoti ya Kamati Kutathmini Hali Vyombo vya Habari wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari Jijini Dar es Salaam.
TIDO: RAIS TUSAIDIE KUPUNGUZA UBABE WA VIONGOZI KWENYE SEKTA YA HABARI
Mwanahabari Mkongwe, Tido Mhando amemuomba Rais #SamiaSuluhuHassan kukemea mazingira ya ubabe wa baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kwenye Vyombo vya Habari kama alivyotoa wito kuhusu Viongozi wa Mikoa kuachana na tabia ya kuongoza kwa ubabe.
Tido ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini Hali ya Vyombo vya Habari ameyasema hayo wakati akikabidhi ripoti ya Kamati yao hiyo wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari Jijini Dar es Salaam
=====
Pia soma:

- Tido Mhando: Awamu ya Hayati Magufuli imechangia 'Comedy Journalism'
- Hii kali: Rais Samia awaagiza JUMIKITA 'kuchuja' maudhui ya mtandaoni tena katika Kongamano la Sekta ya Habari!
- Rais Samia aitaja JamiiForums, asema utoaji wa Habari umehamia mtandaoni kama ilivyo JamiiForums
- Rais anashiriki kongamano la habari huku waandishi wakiendelea kuminywa
- Rais Samia: Kuna mambo Samia hahusiki
- Rais Samia: Vyombo vya Habari sio mshindani wa Serikali bali ni mshirika wa Serikali