Rais Samia akitoa neno moja tu kuhusu wanaohujumu SGR, hakuna atakayethubutu kuharibu tena

Rais Samia akitoa neno moja tu kuhusu wanaohujumu SGR, hakuna atakayethubutu kuharibu tena

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Tumeinvest hela nyingi sana kwenye SGR, jana nimeona kuna watu wamekamatwa wanaiba nyaya, wahujumu uchumi wa wazi, kwa namna tulivyoingia garama, nilitegemea SAMIA atoe tamko moja tu la uhakika ili watanzania wote wasikie na walinde reli hii.

Lakini kwa sababu ya mazoea Watanzania, ukishagharimia mradi kuulinda huwa hawalindi, rais hapo anaweza kuona ameshamaliza kazi, anategemewa kama kiongozi wa nchi atoe tamko juu ya uhujumu huu. Tunamsubiria.
 
Huwezi pewa mke ukapewa na mlinzi wa kukulindia ukiwa unapiga show, lazima utaibiwa tu.... wananchi kazi kumkichwa...
 
Hakuna wizi wa nyaya hiyo ni sanaa tu ya kuwasahaulisha kuzimikazimika kwa used machines tu! Mtanzania gani kibaka mwenye ujasiri wa kuingia na kukata nyanya kwa reli mpya hiyo ambayo muda wote wakaguzi wanapita na kuna umeme, tena akakate kilo 5 hadi 10 tu, mnafanywa mazwazwa tu na mnacheza ngoma ya wapigaji kwa vigelegele na vifijo na mapambio ya kusifu na kuabudu!
 
Back
Top Bottom