Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia akihutubia wananchi Uwanja wa Mkwakwani-Tanga Februari, 2025
Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuangalia uwezekano kuvirejesha viwanda vya mkoa huo ili kuchochea ajira na maendeleo ya kiuchumi. Amesema kuwa miaka ya 1970 na 1980, mkoa huo ulikuwa miongoni mwa mikoa yenye viwanda vingi nchini, ukiwa wa pili baada ya Dar es Salaam.
"Mama tunakuomba utubebe, utushike mkono tufufue viwanda vya Tanga – kiwanda cha chuma, kiwanda cha mbolea, kiwanda cha saruji, kiwanda cha mablanketi na nguo, pamoja na viwanda vya sisal. Vijana wetu, kina baba na kina mama watapata ajira," amesema Ummy.
Mbali na viwanda, Ummy amesisitiza umuhimu wa jiji la Tanga kuwa na chuo kikuu, akieleza kuwa ni miongoni mwa majiji machache nchini yasiyokuwa na taasisi ya elimu ya juu.
"Tulikuwa tunajenga chuo kikuu Tanga, lakini bahati mbaya kikapelekwa wilaya nyingine. Mheshimiwa Rais, Makao Makuu ya Mkoa yanapaswa kuwa na chuo kikuu. Tunapendekeza kiitwe Chuo Kikuu cha Shaaban Robert, ili kuenzi heshima ya mzee wetu wa Tanga."
Rais Samia Suluhu akihutubia wananchi mkoani Tanga
"Namshukuru Mungu kwamba ukichukulia wastani wa upatikanaji wa maji ndani ya Mkoa wa Tanga hatupungui kwenye asilimia 79, 80."
"Niwahakikishie wana Tanga, Barabara ya Tanga - Pangani tutaijenga yote kwa lami. [..]. Aidha lipo pendekezo la kupanua barabara ya Segera – Tanga, tayari tumeanza kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hii na mbele huko tunakwenda kuiweka kwenye ilani na kuijenga."
"Wanaoijua Tanga wanafahamu kwamba hata wahamiaji wengi wa hapa Tanga walikuja kwa sababu ya bandari yake. Tayari tumeanza kuifufua bandari hiyo, mizigo imeongezeka kutoka tani laki nne hadi tani milioni 1.2. Ongezeko hili limeongeza ajira za vijana kwa wana Tanga. Mipango yetu ya baadaye ni kuifanya bandari ya Tanga kuwa maalum kwa mbolea na mazao ya kilimo."
"Kuhusu uwanja wa michezo, tutaanza na maboresho makubwa ya uwanja wa Mkwakwani kwa kuongeza ukubwa wa majukwaa, mara baada ya kukamilisha viwanja vipya vya AFCON 2027."