Rais Samia akutana na Viongozi wa TUCTA, Ikulu ya Dar, Agosti 12, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.

Viongozi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake ya nyongeza ya mishahara, kupandisha madaraja ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya shukrani kutoka kwa Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamhokya kwa kutambua mchango wake katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo, Bw. Tumaini Nyamhokya, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.


​
 
Ukiona mpaka TUCTA nao wamegeuka kuwa chawa! Basi tambua fika ni dalili mbaya sana kwa wapenda mabadiliko. Maana hakuna lililo achwa kwenye jamii mpaka sasa.
We kenge siyo kila kitu ni chawa, wanatimiza wajibu kumshukuru Rais kutekeleza maombi yao. Siyo jambo rahisi kuongeza mishahara kwa kiwango kikubwa kiasi kile tena mwezi wa kwanza wa mwaka wa fedha bila arrears. Samia ni zaidi ya wanaume wawili, ni mwamba.
 
Vipi kuhusu fao la kujitoa kwenye mifuko ya jamii?
Mbona kama hapo kuna dhulma ya wazi wazi na wamenyamazia kimya?
Kweli mtu anaacha kazi akapambane kwenye kilimo na biashara unamwambia asubiri hadi afikishe miaka 55?kweli hii ni sawa?
Miaka 55 atafanya nini na nguvu zinakuwa zimeanza kupungua?
Mama najua ana utu,atuondolee hilo jinamizi lililowekwa na mtangulizi wake
 

Haya mambo ya msingi watu hawayaoni. Fao la kujitoa ni jambo la msingi.
 

Punguza hasira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…