Pre GE2025 Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
We Bwege unaota?
 
Kibajaji ni darasa la saba hajui katiba

Katiba ya CCM inatamka wazi kuwa Mweenyekiti wa CCM ndie atakuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu kumtoa mwenyekiti nje ni ukiukwaji wa katiba na ni mapinduzi ya kumpindua mwenyekiti mchana kweupe
 
Mkwe kapora uchaguzi wa serikali za mitaa. Mama mkwe kapora haki ya wengine kugombea CCM.

Watashirikiana tena uchaguzi mkuu kuiba tena kama kawaida yao wakishirikisha tume, polisi, usalama wana uzoefu wa kutosha sasa.
 
Ni kama JK hakukubaliana na utaratibu, ila ngoja tuone
 
Mama aliwahi kuambiwa kuwa adui zake wako humo humo "Kijani" kwamba akitimiza hoja zetu za Upinzani KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI ugomvi wetu unakuwwa umeisha.
 
Katiba ya CCM inatamka wazi kuwa Mweenyekiti wa CCM ndie atakuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu kumtoa mwenyekiti nje ni ukiukwaji wa katiba na ni mapinduzi ya kumpindua mwenyekiti mchana kweupe

TOKA MAKTABA :

15 Julai 2015
Rais Kikwete alipoendesha vikao vya uteuzi wa Mgombea Urais Tanzania Dodoma


View: https://m.youtube.com/watch?v=NlLkVU7V_cgRais Kikwete alipoendesha vikao vya uteuzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ukumbi wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma Julai 12-13, 2015...


Chama tawala Tanzania mbioni kupata mgombea 2015​

11 Julai, 2015

Rais Kikwete na viongozi wakuu wa CCM
Wingu la kisiasa limetanda mjini Dodoma, Tanzania wakati chama tawala nchini humo CCM kikiwa katika utaratibu wa kuteua mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu wa rais Octoba 25.
Ripoti za hivi karibuni zinasema Halmashauri Kuu ya chama hicho, NEC, imemaliza kikao chake ambacho kilikuwa kinajadili majina matano ya wagombea waliopitishwa na kikao cha awali cha Kamati Kuu ya chama. Vyanzo vya kuaminika vya habari vinasema NEC imejadili majini ya wagombea hao watano – Bernard Membe, Asha Rose Migiro, John Pombe Magufuli, Amina Salum Ali na January Makmaba – bila kuongeza majina yoyote mengine kama ambayo ilikuwa invumishwa.
Baadaye leo usiku, majira ya saa mbili, NEC itatangaza majina ya mwisho matatu na kuyawasilisha kwa mkutano mkuu wa chama ambayo utaanza kikao chake saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Bernard Memba akizungumza na Lowasa wakati wa mkutano wa chama cha CCM

Hali ya taharuki ilizuka kote nchini na hasa mjini Dodoma baada ya Kamati Kuu kutangaza majina matano kati ya watu 32 waliokuwa wakiwania ugombea huo.
Macho zaidi yalikuwa kwa waziri mkuu wa zamani nchini humo Edward Lowassa ambaye aliokuwa anaonekana kama anaongoza katika mbio hizo kutokana na makundi ya watu waliokuwa wakimkaribisha katika mikutano yake ya kampeni za awali kote nchini.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama walijitokeza mbele ya waandishi wa habari Ijumaa usiku na kusema kuwa hawauingi mkono maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu katika kupitisha majina hayo matano.
Wakati huo huo, mwanasiasa mmoja wa upinzani anasema mvutano ndani ya CCM utaongeza nafasi ya muungano wa upinzani kushinda uchaguzi mkuu. Tundu Lissu wa Chadema aliambia VOA kuwa muungano wa vyama vya upinzani, UKAWA, utatumia mpasuko unaojitokeza katika zoezi la kupata mgombea CCM kupata waungaji kutoka chama hicho tawala.

Mikoba yenye makabarasha kwa ajili ya mkutano mkuu wa CCM

Alisema hivyo baada ya Kamati Kuu ya CCM kumwondoa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kutoka kwenye orodha ya wanasiasa wanaotaka kuwania urais kupitia chama hicho.
Wapinzani wake wamekuwa wakimshutumu kwa kugawanya watu na kuhusishwa na ulaji rushwa. Lowassa anakanusha madai hayo.
Kamati Kuu ya CCM ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete anayeondoka madarakani aliondolewa katika majina matano ya wagombea wa awali iliyotangazwa Jumamosi asubuhi.
Wachambuzi wanasema kuondolewa kwa Lowassa huenda kukasababisha mpasuko katika chama hicho, na kuupa upinzani mwanya wa kushinda uchaguzi wa rais.
VoA Amerika
 
Yaan vijana wa uvccm ovyo sana mpka kikwete kawambia " vijana linapozungumzwa jamboa la msingi mtulie na bbadae ndo mshike mabango" na Hawa vijana wamekua wanakurumuka sana pasipo kujua wanakurupukia nn??
 
Kulikuwa na rumours kipindi cha Magufuli kuwa katika yale maongezi aliyorekodi ya kina Membe, Kinana, Kikwete na Mkapa walikuwa wanapanga kumtema asiwe tena mgombea wa CCM 2020 kwa kutumia style hii. Wangemwamabia atoke wajadili jina lake na mara atakapotoka watateua mtu mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…