SI KWELI Rais Samia alipigiwa magoti kwenye kikao alichofanya na wagombea urais

SI KWELI Rais Samia alipigiwa magoti kwenye kikao alichofanya na wagombea urais

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1775128281465.png
 
Tunachokijua
Machi 31, 2026 Rais Samia Suluhu Hassan alifanya mazungumzo na wagombea wa nafasi ya urais na wagombea wenza kutoka vyama vya siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Madai

Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Rais Samia akiongoza kikao huku watu sita wakiwa wamepiga Magoti kumuelekea Rais.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa picha hiyo imepotoshwa kwa kuhaririwa ambapo watu wanaoonekana wakiwa wamepiga magoti wameongezwa kwenye picha kwa kutumia Akili Unde.

Aidha ukurasa wa Ikulu mawasiliano Aprili 01, 2025 umechapisha picha hiyo pasi na watu wanaoonekana kupiga magoti na kueleza tukiola Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na Wagombea wa Nafasi ya Urais na Wagombea Wenza kutoka vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025.​
Back
Top Bottom