Rais Samia alisema aliyegundulika na Marbug ni moja, huyu wa pili ametokea wapi?

Rais Samia alisema aliyegundulika na Marbug ni moja, huyu wa pili ametokea wapi?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Siku ya Jumatatu, Januari 20, 2025 Rais Samia, alithibitisha kuwa mtu mmoja amekutwa na maambukizi ya virusi vya Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera. Leo imetoka taarifa kuwa mtu mmoja kati ya wawili waliobainika na ugonjwa wa Marburg aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo amefariki dunia.

Soma: WHO: Watu nane wamefariki Kagera kwa ungojwa unahisiwa kuwa ni Marburg

Huyu wa pili ametokea wapi au taarifa zinafichwa fichwa kama ambavyo awali iliripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)?

1737717939911.png


Screenshot 2025-01-24 141358.png
Soma, Pia:
 
Tofautisha muda wa matukio
Nitofautishe vipi ikiwa kuna taarifa ya WHO awali iliripoti watu 8 wamefariki na kisha siku kadhaa mbele Rais akasema mtu mmoja anaumwa, huoni taarifa zinachanganya?
 
Wewe Siyo Mgeni Tanzania
WHO Iliposema 8 Wamekufa Haikukosea Ila Tumezoea Ujanja Ujanja
Marburg Dude Lipo, Tena Wajumbe Pale Dodoma Ndiyo Wametawanya Tanzania
 
Ta
Nitofautishe vipi ikiwa kuna taarifa ya WHO awali iliripoti watu 8 wamefariki na kisha siku kadhaa mbele Rais akasema mtu mmoja anaumwa, huoni taarifa zinachanganya?
Taarifa iliyotolewa na Mh. Rais ni baada ya vipimo vya watu waliokuwa wanashukiwa kuwa na ugonjwa huo(Marburg) na mmoja kati ya walofanyiwa vipimo ndyo alikutwa na ugonjwa huo.

Kesi ya waliofariki hakuna aliyethibitisha kwamba waliofariki na ugonjwa huo, labda wewe ndyo utoe hyo taarifa .
 
Back
Top Bottom