Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtahiniwa wenyewe si ndio nyingi mnaoshabikia ccm?sasa mnalialia nini?mkachote maji ziwani.mkiambiwa hiki chama hakifai hamuelewi.pigeni chini hao wabunge wa ccm lina bado mnawakumnatia sasa mpambano na hali zenu.chimbeni visima.Mimi Mkazi wa Geita kwa muda mrefu sasa mkoa wetu umekuwa na changamoto ya mgao wa maji.
Maji yamekuwa yakitoka mara moja kwa wiki. Hii ni kwa Mtaa wetu na maeneo mengine mengine.
Kila tukiuliza shida ni nini viongozi wetu wamekuwa wakitoa visingizio. Kila mara wamekuwa wakisema kuwa wapo kwenye mchakato wa kutengeneza mfumo na kutanua mtandao wa maji
Ajabu ni kwamba juzi hapa wakati Rais Samia alipotutembela Wanageita katika ziara yake maji yalikuwepo vizuri tu.
Maji yalikuwa yanatoka na tulipata maji karibu sehemu zote, maji yalikuwa yanamwagika, karibu sehumu zote maji yalikuwepo lakini baada ya Rais kuondoka na maji nayo yakaondoka hayakutoka tena.
Kiukweli kabisa tunapata shida. Imefikia hatua tunanunua maji dumu moja 500 au 1,000 mpaka 1500.
Sasa hiki wanachozungumza viongozi ni ukarabati na matengenezo gani yasiyoisha? Ninachojiuliza mimi na wenzangu ni kuwa Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) kwani shida ni nini?
Baadhi yenye changamoto ni Mtakuja Mwatulole, Nyankumbu, wale wanaopata nafuu wao wanapata maji ya bomba mara moja kwa wiki.
Pia, soma: √ - Tatizo la Maji kwa Mji wa Geita kuwa Historia kufikia Oktoba 2025