Rais Samia Suluhu Hassan amepiga simu kwenye pambano la #KnockoutYaMama (KO ya Mama) na kuwapa salamu za Sikukuu ya Krismasi na kuwatakia mwaka mpya mwema mashabiki waliofurika kwenye ukumbi wa The Super Dome, Masaki kushuhudia pambano hilo.
Katika salamu zake, Rais Samia pia aliwataka mabondia Watanzania kupambana na kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
Katika salamu zake kwa mamia ya mashabiki wa ndondi na mabondia ukumbini hapo, Rais Samia ambaye alieleza kulifuatilia pambano hilo laivu amesema, kilichompa hamasa ni jina la mchezo la Knock Out ya Mama.
"Wosia wangu mcheze vizuri, sheria zifuatwe," amesema Rais Samia alipokuwa akizungumza na mashabiki ukumbini hapo ambao muda wote walikuwa wakimshangilia.
Awali, Rais alianza kwa kumtania Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mgeni rasmi na kumueleza alikuwa na wasiwasi wasimweke yeye Waziri mkuu ulingoni, utani ulioamsha shangwe kwa mashabiki huku waziri mkuu pia akitania kwamba amewahi kuwa bondia.
Pia amewasihi Mabondia wa Kitanzania kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mapambano yao.
Samia na majaliwa shikAmoo, ngoja niwaangalie umri wao. Mie sitoi shikAmoo labda mtu awe ananizidi 18 zaidi Mana huyo ananizaa otherwise ni dada ama kaka zangu hao nimekua nao
Kassim Majaliwa Majaliwa (born 22 December 1960)
Samia Suluhu Hassan born 27 January 1960).
Hawa wanalingana yaani ni Ile kuishi kwa ku fake ,Nina Imani majaliwa hatoi shikAmoo kwa aliyemzidi 5yrs hapo akasalimia cheo Ila sio mtu