voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Kati ya watu walio kwenye kumbukumbu ya kuutaka urais.
Mwigulu Nchemba Madelu, ni mmojawapo,na ushahidi bado maandishi yako kwenye mawe katika barabara kuu nyingi yakisomeka
"mwigulu for president".
January Makamba, ni mmojawapo wa viongozi waliokuwa wakiratibu kampeni za mtandaoni huko Twitter, wakiratibu kundi la Membe, ingawa baadae na yeye aliweka jina lake.
Na uteuzi wake kurudi wadhifa wa waziri wa nishati umegubikwa na madudu tupu. Tangu ameingia Tanesco imerudia ile enzi kama iliyopelekea kuleta kashfa za Dowans na Richmond kisha IPTL.
Nape Nauye, huyu alijulikana wazi kuwa kambi ya Membe mpaka dakika ya mwisho na mpaka leo ubunge wake kule mtama mratibu wake mkuu alikuwa Membe.
Uteuzi wake kurudi wizara ile ile una walakini, aidha kuna mpango maalum wa kulipiza visasi kwa walengwa fulani kutoka team inayoondolewa kwa kasi, hilo ni suala la muda na tutayaona mengi.
Ni hivi karibuni alinukuliwa akisema CCM ina wenyewe, je wanaomshauri rais hawakuona maneno hayo pekee yana uzito fulani kwa umoja na mshikamano wa chama?
Kumrudisha hapo tayari kunapelekea baadhi ya wananchi kuamini kwamba sasa CCM iko mikononi mwa kikundi cha watu wachache wenye nia na madhumuni binafsi.
Wako weengi huko wenye tunawajua, ambao tamaa na uchu wao wa urais sio siri kwa watanzania tulio na ufuatiliaji wa siasa za nchi hii.
Hawa maskini wa kizalendo wametoswa na kundi msoga kutokana na kuonekana mwiba kwao.
Lukuvi - Mungu akujalie nguvu na afya njema ili uyaishi na kuyaona yatakafuata.
Ikiwezekana chukua fomu ya uspika ,kama system isipokufanyia figisu, nina imani na wewe kama ilivyo kwa watanzania wengi nchini.
Huenda nyota yako ikaendelea kun'gaa.
Kabudi...wewe mtaaluma na mbobezi uliyebeba historia nzuri ya nchi hii.
Wasomi wa kariba yenu wanaendelea kupungua nchini.unao uwezo wa kuitumikia wananchi wa jimbo lako la ubunge na ikiwezekana tafuta wafadhili muingie ubia na ufunguwe taasisi ya elimu ili utuachie ujuzi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Mwambe...Uliteleza siku unajibu swali kuhusu bandari ya Bagamoyo.
Jambo lilopelekea kuibua hisia hasi na kali kwa wananchi dhidi ya huo mradi.
Jambo ambalo limewakasirisha wenye mradi wao.
Waitara...sina uhakika hasa kama wewe una ndoto za urais ila huenda mama hapendi wapiga Gambe,mfano tuliona akimuadhibu Polisi aliyetoa clip miaka 3 huko nyuma. Ila akaamuru afukuzwe kazi juzi.
Mungu tuvushe salama