benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Marekani imeahidi kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha uchumi na maendeleo ya wananchi kwa kutoa fedha na ujuzi pamoja na kuvutia uwekezaji kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi.
Ahadi hiyo imetolewa na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, katika Ofisi Ndogo za wizara hiyo, Dares Salaam, alipofika kujitambulisha.
Battle amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kusimamia na kukuza uchumi wa nchi na kuamua kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika bajeti yake kwenye sekta za uzalishaji zinazogusa Maisha ya watu kikiwamo kilimo.
"Tunaahidi kuwa Marekani itaendelea kuiunga mkono serikali ya kiongozi shupavu ambaye si tu kwamba anapigania sana maisha ya Watanzania, lakini pia amekuwa mwanadiplomasia anayepigania maendeleo na utangamano wa Afrika,"alisema Balozi Battle.
Balozi Battle alisema Rais Samia Suluhu Hassan amegusa mioyo ya Wamarekani na viongozi wake ndiyo sababu za Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris kupanga ziara ya kuitembelea Tanzania, ambako viongozi hao wawili watafungua fursa zaidi za ushirikiano