Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
RAIS SAMIA AMEIBEBA AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KIMATAIFA
Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) katika Msimu wa Kizimkazi Festival tarehe 23 Agosti, 2024 iliandaa Mdahalo wa Nishati Safi ya Kupikia ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia nchini na Afrika bado anaendelea kuipeleka ajenda hiyo Kimataifa ili kuhakikisha watu wanapika katika mazingira salama kiafya na kimazingira.
"Matarajio yetu ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia. Nimefarijika sana kuona utekelezaji wa lengo hili kwa vitendo, nimeona teknolojia mbalimbali katika mabanda ya maonesho hapo nje na niendelee kuhamasisha ubunifu wa teknolojia zinazowezesha wananchi kupata nishati safi kwa gharama nafuu" Dkt. Biteko
Aidha, Mhe. Wanu Hafidh Ameir akizungumza katika Kongamano la Nishati Safi ya kupikia Zanzibar amebainisha kuwa lengo ni kuhamasisha ubunifu katika teknolojia za Nishati Safi ya Kupikia.
Mhe. Wanu Hafidh Ameir ambaye ni Mbunge na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) amewashukuru Benki ya Uwekezaji ya Tanzania (TIB) kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi zote za Serikali kuwezesha Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika katika Hoteli ya Kwanza, Kizimkazi Zanzibar.
Vilevile, Mhe. Wanu Hafidh Ameir amepongeza ubunifu kutoka ORXY ambao umekuja na ubunifu kwenye mitungi ya gesi (LPG) kwa kuweka mita inayopima gesi ambayo inarahisisha gharama za kujaza gesi na kuwa nafuu zaidi
#KizimkaziFestival2024
#KizimkaziImeitika