Rais Samia amelipia ticket 5000 za Mashabiki watakaokwenda kuishangilia Yanga fainali ya CAF, 28/5/2023

Rais Samia amelipia ticket 5000 za Mashabiki watakaokwenda kuishangilia Yanga fainali ya CAF, 28/5/2023

Kwa upendo mkuu Rais Samia amewanunulia ticket Mashabiki 5000 watakaoenda Uwanja wa Mkapa kuishangilia Yanga dhidi ya USM Alger

Source: Azam tv
Ni jambo zuri sana alilolifanya Rais wetu Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan, lakini hao mashabiki waliolipiwa hizo tiketi wamepatikana kwa njia ipi, asije akapigwa changa la macho na wajanja wa mjini, nadhani hili lingekuwa na uwazi zaidi.
 
naamkaje sasa, kwa hayo mawazo mgando yenu, kwamba yeye hapaswi kuwa shabiki na kufanya lolote katika mpira, mfano chukulia kwamba rais analipwa M 150 kwa mwezi (mimi sijui kama rais ana mshahara)...

tiketi 5000 kwa ghrama ya 10000 kila tiketi maana yake ni kiasi cha m50 tu ndio kitatumika (5000*10000), sasa kama ana mapenzi ya mpira na kaamua kutoa robo ya mshahara wake kuna tatizo..??
Mshahara wa raisi ni 9M labda kama amwjiongezea Kimya kimya
 
Huyu maza anachefua sana sana tena sana!!!!!! kuna shule hazina hata madawati.....
 
samia anakisima cha mafuta wenda, maana nakumbuka tajiri mmoja wa manchester city alikata tickets za watu 6000 bure
 
Assume tiketi ni 10,000
Jumla ni 50,000,000 hapa angeweza hata kuwainua vijana zaidi ya 10 na kuwapa mtaji wakajikwamua kimaisha.

“They got money for Soccer, but can’t feed the poor” [emoji119]
Kwani hao wanaoenda huko sio vijana mbon mnapenda kuponda kila kitu, mfunze Mwanao apende soccer sasa na wewe unufaike na soccer kwani lazima wote tuwe mainjinia ?
 
Huyu maza anachefua sana sana tena sana!!!!!! kuna shule hazina hata madawati.....
Shule hazina madawati nyinyi hamna viongozi ? Yeye atapita kila shule kukagua madawati ? Umesikia hio ndio kazi yake kukagua madawati ya shule ? Hua mnawaza nini mnapouliza maswali ya kijinga ? Umeona shule haina madawati anza na afisa elimu Kata nenda kwa afisa elimu Wilaya nenda na afisa elimu wa Mkoa nenda Halmashauri nenda kwa mkuu wa Mkoa fuatilia mpaka kwa Diwani wako na Mbunge wako uliemchagua we umeikalia kuna shule hazina madawatiiii.... Fyoko
 
kwani hawezi tumia pesa yake ya mshahara ama posho..??
Okay, na mafuta ya ndege ya kumsarisha Hayati Le Mutuz nayo Mama Samia katoa mfukoni mwake?

Na yule mfanyakazi wa ofisi ya Vice President na mtoto wa Mabeho na marehemu wote mashuhuri Rais anatoa hela ya mafuta ya ndege mfukoni mwake!

wanatucheka sana hawa viongozi, wameshajua raia wenyewe nao viaziiiiiiiii... mtu anasema "kwani amesema kwamba hii ni priority" ? yani mpaka rais atamke kwamba hii ni priority yangu ndio tujue priority za huyu Mama ziko upside down...
 
Back
Top Bottom