Rais Samia amemtumia pongezi Rais Mteule wa Zambia, Hakainde Hichilema

Rais Samia amemtumia pongezi Rais Mteule wa Zambia, Hakainde Hichilema

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa Tanzania amemtumia pongezi Rais mteule wa Zambia Mheshimiwa Hakainde Hichilema na kumuahidi ushirikiano.

Naye Rais MTEULE Mheshimiwa Hakainde amezipokea pongezi hizo na kumshikuru Rais Samia huku akimuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu kwani nchi hizo mbili zina masuala muhimu yanayowaumganisha hivyo mahusiano yao yanapaswa kuwa imara zaidi.

Kazi Iendelee.

IMG-20210817-WA0002.jpg
 
Anaapishwa lini? Bombardier imeshajazwa mafuta na ushungi mpya umeshanunuliwa.
 
2025 CCM imekwisha, waTanzania wapongezwa kwa kupata kiongozi mpya asiyetokana na CCM. Je ni sababu gani zitawafanya waTanzania kuchukua hatua hiyo:
  • Uchovu wa ndani ya CCM kufanya siasa kutokana na kutenda maovu tangu siasa za vyama vingine kuanza 1992. Mfano gazeti la UHURU kuonesha kuchoka huku mhariri wake mkuu wa gazeti pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM MNEC.
  • Kila mtanzania akiangalia matendo ya CCM wanaona ni eneo la jinai yaani Crime scene mfano tozo za miamala, miradi ghofu ndege za Air Tanzania , SGR reli mpya, Stiegler's gorge, kesi za kubambikia, wafungwa wa kisiasa, matumizi mabaya ya vyombo vya usalama n.k
  • Makada na wanachama wa CCM wamekuwa kundi kubwa la watesi kwa waTanzania
  • Kujiunga na CCM ni chuo tosha kuufanya watanzania waanze kujiuliza msimamo wako ni upi mfano Humphrey Polepole na wengine kubadilika ghafla wanachoamini
  • Wananchi kutambua kuwa hawana wawakilishi wao waliowachagua kupitia uchafuzi wa uchaguzi wa wabunge, madiwani, wenyeviti wa Mitaa na Vijiji. Hivyo kifupi hawana viongozi waliowachagua wao.
Kinachofuata ni kuwa 2025 hawatakichagua chama-ruhani cha CCM kwa kuwa CCM hakina tena vinasaba / DNA ya sifa za kuwa chama cha kisiasa.

Wananchi wataamua kujirudishi madaraka kwa kukubwaga chama cha CCM na wagombea wa CCM ili wapate viongozi na serikali halali watakayoweza kuiwajibisha ikifanya vibaya pia kuwa na wabunge pamoja na wawakilishi watakao ingia Bungeni kutetea wananchi wakitakacho.

Mwaka 2025 kwa mara ya kwanza, tutapokea pongezi kwa kuwa na serikali nyingine isiyo ya CCM baada ya wananchi kuikataa CCM kupitia box la uchaguzi.
 
Aandaye ushungi mpya ili kwenda kuhudhuria kuapishwa
 
Back
Top Bottom