mjizu123
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 349
- 369
Rais wa nchi, Mh. Samia Suluhu Hassan, ameonesha Ukomavu na Utayari mkubwa katika kuleta mabadiliko ya mfumo wa utawala wa Taifa letu pamoja na changamoto kibao zinazolikumba Taifa hili kwa sasa na kipekee sana wahafidhina ndani ya Serikali na chama Tawala ambao wanajaribu kukwamisha au kuchelewesha mabadiliko hayo kwasababu ya maslahi yao binafsi.
Itoshe kusema kwamba, kulingana na historia na utamaduni wa Mfumo wa uongozi na Utawala wa nchi hii baada ya kuondoka kwa Mwl. Nyerere madarakani mwaka 1985, ni tukio la ajabu na kushangaza kwa kiongozi wa Juu kutoka chama Tawala (CCM) na serikali hususani ambae ni Rais wa nchi kuruhusu na kutoa fursa chanya ya kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo ambayo yanaweza kuwa ndio silaha (Tishio) kubwa dhidi ya uhai wa chama Tawala kuendelea kubakia madarakani.
Utawala wa CCM umekuwa na ngao kubwa mbili za kuhakikisha kwanza chama hicho kinaendelea kutawala nchi hii (libakie madarakani mileme), pili kinaendelea kulinda maslahi yake, hii ikiwa ni pamoja na kulinda wafadhili wake dhidi ya matishio yoyote yale ya ndani na nje ya chama na serikali ikiwemo wala na watoa Rushwa wakubwa. Kwahiyo Uamuzi na msimamo wa mama kuruhusu mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya na mabadiliko ya sheria.
Kadhaa kandamizi ni jambo la busara na la kupongezwa na kama tutafika mwisho salama tofauti na ilivyokuwa wakati wa Mzee Kikwete basi anaweza kabisa kuweka rekodi ya kipekee sana ktk viongozi waliowahi kutawala Taifa hili baada ya Mwl. Nyerere.
Lakini, pamoja na Utashi huo wa mama na Utayari wake, bado ameonesha udhaifu mkubwa katika kushughika na Wabadhirifu wa Mali za umma pamoja na mamlaka makubwa alionayo katika katiba hii ya sasa na sheria zake, katika kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi zilizopo. Ripoti ya CAG imerejerea ubadhirifu mkubwa zaidi kwa mwaka mwingine wa bajeti ya serikali lkn tunashuhudia Rais wakilalamika na kusuasua katika kuchukua hatua za haraka na kubwa za kuhakikisha Rushwa inatafsiriwa kivitendo kuwa adui wa jumla wa haki Tanzania pamoja na kurejeshwa kwa mali za nchi.
Ni maoni yangu kwamba, Mama akamilishe mchakato mzima wa mabadiliko ya mfumo wa Utawala kabla ya 2025, then tupate kiongozi mpya mwenye uwezo wa kusimamia Sheria na Katiba mpya ili kujenga utamaduni mpya wa Tanzania na watawala kuheshimu sheria za nchi na kama msingi wa kulinda rasilimi za Taifa hili.
Pili, tupate kiongozi mpya ambae kupitia Katiba na sheria mpya awe mwenye uwezo wa kuchukua hatua kali na kwa wakati za kudhibiti wizi na ufisadi wa mali za umma ili kila mwanachi wa Taifa hili aone faida ya uwepo wa serikali mbali ya faida ya jumla ya udhibiti wa rushwa na Ufisadi nchini. Rais ajae anapaswa kuwa mtu ambae hata ukimtizama, basi anaonesha anachukia Rushwa.