Bibititi1
JF-Expert Member
- Sep 28, 2014
- 464
- 218
MAMA NI MLEZI… .
Ndugu zangu acheni leo tuseme mazuri juu ya Mama yetu kipenzi na Mlezi wa Taifa hili Amri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mama mengi mazuri ametimiza ndani ya muda mfupi, Wengi tunajua Maisha yetu yalisimama wima kama maghorofa ya kariakoo. Mifuko yetu ilikuwa mitupu na matumbo yalikuwa yakiitika labekaa kwa njaa.. “tulikuwa tunatembea kwa kuinamisha kichwa chini hadi shingo ikapinda kama mforosadi”
Bongo Movie ilikuwa kilio, Bongo fleva kilio, Walimu kilio, Watumishi wa umma kilio…Nchi iliishi kwenye msiba wa ukata na ukosefu wa furaha maana matajiri nao waliishi kama mashetani. Jiji hili la Dar es salaam moshi wenye harufu ya kuudhi ulilelea hewani ukitamalaki kwenye majumba yetu kujiuliza kesho zamu ya nani kuishi kama shetani.
“Nitasema nitasema!” acheni niseme mimi, Asiposema Steve nani wa kusema wakati napata wazo la Mama Ongea na Mwanao nilijua itafika siku Mama atasimama na taifa hili kulifuta machozi kwenye kila nyanja kwenye kila sekta itakuwa ni furaha.
Leo tunaona kweli nchi inafuraha pia mwangaza unaonekana Mhe Rais Kuhudhuria tamasha la mwanamuziki wa Hip Hop tena mfuasi wa chama cha Upinzani na viongozi wote kwa pamoja wakajumuika wa pande zote mbili. Hili limeta umoja wa kitaifa tena kuwa sisi ni ndugu wa damu moja tofauti za nini. Mama ana show love to each other.!
Embu tumpongezeni Mama kwa haya machache ametoa ruzuku ya mafuta ya Petrol na Dizeli leo bei ilikuwa ifike elfu tatu na mia tano 3500 yaani ingepaa juu kama Paa lakini Mama kwa huruma zake na upendo wake kwa taifa hili ametoa ruzuku zaidi ya bilioni 100 imefika shilingi Elfu mbili na kenda kadhaa nchi imejinyima kwa ajili ya wananchi wake waliosema haiwezekani leo wamefunga midomo kama mabakuli ya pombe na wamenyanyua mabega juu yanakaribia kukutana na masikio.
Mwaka 2015 Tulimuamini Mama tukazunguka naye nchi nzima. Imani yetu Tulifahamu siku zote Mama ni Mama yeye hukusanya si mtawanyaji huwaleta watu karibu zaidi na Hiyo ndiyo maana ya kuijenga nchi miaka zaidi ya sita kaka yangu Mbowe alikuwa anaonekana kama mkimbizi alipoteza mashamba, Disko lake lile pale pamekuwa kituo cha Tax na kidogo angekuwa kilema. Ndugu yangu Sugu aliambiwa hotel yake amejenga kwenye chanzo cha maji utanzania ulifutika kabisa.
Furaha ilikata kona na kupotea kabisa si kwa watumishi wa Umma si kwa sekta binafsi, Furaha ilienda uhamishoni. Kwa mara ya kwanza tangu uhuru gridi y a Taifa ya umeme Inafika Kigoma kabla ya mwezi wa kumi mwaka huu wenzetu walikaa gizani muda ila Mama leo ametimiza. Unaambiwa sasa Kigoma tutakuwa tunakwenda asubuhi mchana tupo DAR hapa tunakula migebuka Treni ya umeme na umeme wa uhakika upo.
Wapo watakaosema eti steve usiseme hivyo! Tusiposema kuwa wafanyakazi wameongezewa mshahara ni kosa? Tusiseme wafanyakazi wameongezewa posho ni kosa, Tusizungumze wastaafu wamepata kikotoo kipya cha mafao. hawa watu makoo yao yaliwasaliti kwa muda mrefu wacha wafaidi matunda ya jasho lao.
Huyu ndiyo MAMA Tulimuomba aongee na wanae ametusikia anazungumza na sisi kwa vitendo amefanya Royal Tour kwa ajili ya kukuza utalii, Amelipa madeni makubwa ya Serikali zaidi ya Trilion 11, Ametoa mirabaha kwa kazi za wasanii, ameongeza bajeti kwenye miradi ya maji, barabara na afya kama haitoshi amejenga madarasa zaidi ya elfu 15,000 nchi nzima hakuna mwanafunzi aliyekosa kuingia darasani mwaka huu wa masomo. Nchi imefunguka wawekazaji kila kona juzi tumeona meli imetia nanga bandari ya Mtwara inabeba makaa ya mawe kutoka Ruvuma.
Wacheni nisemeee mie…. Mama ameongea na wanae kwa vitendo.