Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais, Dkt. Samia ameyasema hayo Agosti 05, 2024 wakati akihitimisha ziara yake katika Mji wa Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambapo amesisitiza kuwa uongezaji thamani wa bidhaa katika viwanda unahitaji uwepo wa umeme wa uhakika hivyo Serikali inafanya kila jitihada ili nchi iweze kujitosheleza na nishati hiyo na kuwezesha uongezaji thamani malighafi zinazopatikana nchini ikiwemo mazao.
Ameongeza kuwa, kupatikana kwa umeme katika maeneo hayo kumeendelea kuwavutia wawekezaji wa ndani ambao wameweka mashine za kuchakata nafaka na kuongeza kuwa ujenzi mkubwa wa maghala unaendelea.
"Uwekezaji huu unaonesha kwamba umeme umeleta faida kubwa ndani ya maeneo haya, niwahakikishie Serikali itaendelea kusimamia Sekta ya Nishati ili kuendelea kuwa na umeme wa uhakika," amesisitiza Dkt.Samia.
Akizungumzia miradi ya umeme vijijini, amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeshapeleka umeme kwenye vijiji vyote 110 vya Wilaya ya Kilombero.
Ameongeza kuwa kazi inayoendelea sasa ni upelekaji wa umeme kwenye Vitongoji na kwenye Taasisi.