Rais Samia amteua Mkuu wa Jeshi la Magereza

Rais Samia amteua Mkuu wa Jeshi la Magereza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
WhatsApp Image 2024-07-29 at 18.53.48_1176917f.jpg


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkuu wa Jeshi la Magereza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Kamishna wa Magereza CP. Jeremiah Yoram Katungu amepandishwa cheo kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza.

CP Katungu anachukua nafasi ya CGP Mzee Ramadhani Nyamka ambaye amestaafu.

Uteuzi huu umeanza tarehe 28 Julai, 2024.
 
Rais Samia amemteu CP Yoram Katungu kuwa MKUU MPYA WA MAGEREZA baada ya CGP Ramadhan Mzee kustaafu.

IMG-20240729-WA0035.jpg
 
Back
Top Bottom