Rais Samia Amuapisha Zuhura Yunusi kuwa Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

Rais Samia Amuapisha Zuhura Yunusi kuwa Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Hii leo June 13 Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, Akiwa katika Ikulu ya Chamwino Dodoma amefanya uapisho wa viongozi mbalimbali aliowateua siku chache zilizopita.Uteuzi ambao uliteka mijada mbalimbali ya kisiasa hapa Nchini.

Ambapo katika uapisho huo ameweza Kumuapisha Mheshimiwa Zuhura Yunusi Abdallal kuwa Naibu katibu mkuu ofisi ya waziri Mkuu(kazi, vijana, ajira na wenye Ulemavu), Muandishi na mtangazaji Nguli aliyefanya kazi kwa mafanikio makubwa sana katika kituo cha utangazaji cha BBC Uingereza, na kujijengea heshima kubwa sana Duniani kwote .kutokana na umahiri wake wa kutangaza na kusimamia maadili ya taaluma yake.

Zuhura Yunus.jpg

Mheshimiwa Zuhura Yunus Abdallal kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu,kazi aliyoifanya mpaka June 6 alipobadilishiwa majukumu na kuhamishiwa katika nafasi ya Unaibu katibu Mkuu wa ofisi ya Rais(kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu). Nafasi ambayo naamini ataifanya kwa ufanisi Mkubwa na kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais kumpatia nafasi hiyo.hasa kwa kuzingatia kuwa ni wizara inayowagusa vijana ambalo ndilo kundi kubwa hapa nchini.

kundi linalohitaji kuangaliwa kwa jicho la kipekee kabisa kisera ,kibajeti na kisheria,kwa kuhakikisha kuwa sera zinazotungwa zinalipatia kipaombele na kulipatia matumaini bora na hai katika ustawi wao. Mheshimiwa Zuhura ni mtu aliyeishi Ulaya na naamini anajuwa na kuelewa Dunia inakwenda vipi na nini Kiu ya vijana .hasa kwa kuzingatia UKWELI kuwa ni Msomi mzuri na hivyo naamini atawasaidia vijana wengi sana kupata fursa kupitia sera mbalimbali pamoja na kuwafungulia DUNIA vijana.hasa wakati huu ambao Dunia inapambana na changamoto hii ya ukosefu wa ajira kwa vijana.

Nakutakia kila lenye heri Mheshimiwa Zuhura Yunusi Abdallal .kafanye kazi kwa bidii ,juhudi na maarifa ili kuleta matokeo chanya kwa vijana.lakini kubwa kuliko yote ni kuwa shirikiana na kila mtu lakini usimuamini mtu yeyote yule .Narudia kukuusia kuwa shirikiana na wote lakini usimuamini mtu yeyote yule.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

=====

Pia soma: Rais Samia afanya uteuzi na mabadiliko ya watendaji wa Serikali. Zuhura Yunus aondolewa Ukurugenzi wa Mawasiliano Ikulu
 
Naamini anajuta kuacha kazi kule BBC London. Lol
Poleee yake bibi. Woiiiiiih
 
Mleta mada unamkebehi Zuhura Yunus ujue huku unampigia debe Kafulila unajua unajitengenezea maadui

Zuhura Yunus alikuwa anasafiri na Raisi kutwa nje ya Nchi analipwa madola posho za safari Leo kapata cheo Cha kushinda nchini tu kusibiri mshahara wa mwisho wa mwezi pesa za Tanzania

Halafu wewe unaleta kebehi zako eti nampongeza Zuhura Yunus kuondoka namkupiga debe Kafulila achukue nafasi yake

Kwani ungekaa kimya ungeumwa malaria?
 
Mleta mada unamkebehi Zuhura Yunus ujue huku unampigia debe Kafulila unajua unajitengenezea maadui

Zuhura Yunus alikuwa anasafiri na Raisi kutwa nje ya Nchi analipwa madola posho za safari Leo kapata cheo Cha kushinda nchini tu kusibiri mshahara wa mwisho wa mwezi pesa za Tanzania

Halafu wewe unaleta kebehi zako eti nampongeza Zuhura Yunus kuondoka namkupiga debe Kafulila achukue nafasi yake

Kwani ungekaa kimya ungeumwa malaria?
Acha utoto wako kwenye masuala ya msingi.
 
Back
Top Bottom