Rais Samia anaandika historia ya kipekee katika mapinduzi ya kilimo

Rais Samia anaandika historia ya kipekee katika mapinduzi ya kilimo

msuyaeric

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
842
Reaction score
1,197
Ajenda ya 10/30 inayobebwa na kauli ya KILIMO BIASHARA inatekelezwa kwa kasi ambayo kila mtanzania ni shuhuda. Rais Samia ameonyesha uhalisia kuwa inawezekana, haya ni baadhi ya mambo yanayofanyika hivi sasa.

Tayari Hekari 11,453 zimetengwa kwaajili ya mradi wa vijana (Block farms) katika Mkoa wa Dodoma na mpango wa Hekari 23,144 uko mbioni kutekelezwa Mkoani Njombe. Hii ni sambamba na Fedha takribani Bilioni 150 ambazo zimetengwa kuwasaidia wakulima ikiwa ni pamoja na kushusha bei ya Mbolea kwa zaidi ya 50%.

Serikali imeweza kuongeza bajeti ya huduma za Ugani kutoka TZS bilioni 17.7 hadi TZS bilioni 51.45, kuongeza fedha za uzalishaji wa mbegu kutoka TZS bilioni 5.42 hadi TZS bilioni 10.58, sambamba na kuongeza bajeti hiyo, Rais Samia amewezesha NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kwa jumla ya TZS bilioni 129 ili waweze kuongeza ufanisi.

IMG-20220817-WA0056.jpg
IMG-20220815-WA0300.jpg
 
Back
Top Bottom