Rais Samia anafungua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) - Ubungo, leo Agosti 1, 2025

Rais Samia anafungua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) - Ubungo, leo Agosti 1, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Samia Suluhu Hassan Akifungua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) Ubungo Dar es Salaam, leo tarehe 1 Agosti, 2025.


View: https://www.youtube.com/live/khT-HcF4C3w

WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.27_0c566c0f.jpg

WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.36_148d8a55.jpg

WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.31_7297aeb0.jpg

WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.42_6dc69120.jpg

WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.22_f960b6db.jpg

WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.23_4e81f2aa.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Akifungua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2025.
WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.29_c4b5f6fa.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2025.
WhatsApp Image 2025-08-01 at 13.44.38_ef2daac0.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea maduka yaliyopo katika Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2025.
​

EACLC NI USHAHIDI WA MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA KWENYE UWEKEZAJI
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Bw. Gilead Teri, amesema kuanzishwa kwa mamlaka hiyo ni moja ya mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, na kwamba sasa Tanzania imefungua ukurasa mpya katika kuvutia mitaji na kukuza ajira kupitia miradi mikubwa ya kimkakati.

Akizungumza tarehe 1 Agosti 2025 mkoani Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (East Africa Commercial and Logistics Centre – EACLC), Bw. Teri amesema TISEZA ilianzishwa rasmi Julai 1, 2025 baada ya Bunge kupitisha Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Na. 6.

Kuhusu mradi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki, Bw. Teri amesema umetumia zaidi ya shilingi bilioni 282.7 hadi hatua ya kukamilika, tangu ulipoanza kutekelezwa Mei 2023. Mradi huo una jumla ya vizimba 2,060 vinavyokaliwa na wafanyabiashara wa aina mbalimbali, na ujenzi wake umetengeneza ajira zaidi ya 2,000.

“Baada ya kukamilika, tunatarajia ajira zaidi ya 15,000 za moja kwa moja, na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 50,000. Eneo hili lina ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 75,000”, amebainisha Teri.
 
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kufungua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC)

📆 01.08.2025
🕰️ Saa 5 Asubuhi
📍Ubungo, Dar es Salaam

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia Akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel: Ikulu Tanzania na Tovuti: www.ikulu.go.tz
 

Attachments

  • IMG-20250801-WA0153.jpg
    IMG-20250801-WA0153.jpg
    221.6 KB · Views: 44
Back
Top Bottom