LGE2024 Rais Samia anapanga foleni ya kujiandikisha ila tunakaa masaa matatu barabarani kusubiri msafara wake upite!

LGE2024 Rais Samia anapanga foleni ya kujiandikisha ila tunakaa masaa matatu barabarani kusubiri msafara wake upite!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

RAIS DKT. SAMIA NI KIONGOZI WA MFANO, APANGA FOLENI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA

Ikiwa Kiongozi ni mfano basi Leo Watanzania wanajifunza jambo lingine kubwa kutoka kwa Kiongozi wao mpendwa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akijindikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa kwenye Kitongiji chake cha Sokoine kilichopo katika Kijiji cha Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma leo tarehe 11.10.2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza watanzania katika zoezi la Kujiandikisha katika Daftari hili ili kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.10.jpeg
    117.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.11(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.11(1).jpeg
    260.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.11.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.11.jpeg
    207 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.12(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.12(1).jpeg
    45.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-11 at 20.41.12.jpeg
    192 KB · Views: 2
Sawa. Atukumbuke na sisi tuliopanga foleni kusubiria ajira. Maana kozi zetu huwezi kujiajiri.
 
Naona Mama amekaa foleni ya usalama wa Taifa wengine wamejivesha nguo chakavu kasoro huyo Tall kashindwa kujiweka tofauti na kazi yake..
 
Back
Top Bottom