Rais Samia anashindwa kuongea na Upinzani kwakuwa umenyambu. Je, ni kweli upinzani umenyambuka?

Rais Samia anashindwa kuongea na Upinzani kwakuwa umenyambu. Je, ni kweli upinzani umenyambuka?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Hata Rais anashindwa kuongea na wapinzani kwakuwa wamenyambukanyambuka, hajui aongee na nani.

Je, ni kweli wapinzani mmenyambukanyambuka? Kumuona Mbowe pekee akiwa kwenye kurasa za mbele za magazeni ndio ukweli kuwa mmenyambukanyambuka?

Zitto, Mbatia, Lipumba, Rungwe na wapinzani wengine wapendekeze Njia mbadala na rahisi ya kupata tume huru ya uchaguzi inayokubalika kwa wapinzani kabla 2025, maana muda unakwenda kuelekea 2025.
 
Huyu Mama sasa hata anachoongea hakijui!

Chama cha Chadema ndiyo pekee kilichotuma maombi rasmi ya kukutana na Rais Samia, sasa yeye anapotaka kuwaunganisha na kina Mrema wa TLP na Profesa Lipumba wa CUF, ni kutaka kuwakutanisha wapinzani halisi na vyama vya siasa vya upinzani lakini Katika muundo wao ni CCM-B!

Najua Rais Samia anataka kutumia mbinu ya "divide and rule"
 
Mama usikubali CHADEMA wakupangie tafadhali sana wewe ni president una kila rasilimali iwe watu, vitu
 
Mama akutane na kila chama kwa namna yake kwa sababu ajenda za Chadema sio za NCCR, wala ajenda za ACT sio za CUF n.k

Unapotaka kukutana na ZItto, Lipumba, Mrema n.k kwa wakati mmoja kwa maana kwamba watu hao wawe wameafikiana kuwa na kauli moja ni ngumu...
 
Vyama vya siasa vinaongozwa na matakwa ya mtu na siyo Katiba tena.
 
Back
Top Bottom