Rais Samia anatarajiwa kufanya Ziara Mkoani Simiyu pamoja na kuzindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo

Rais Samia anatarajiwa kufanya Ziara Mkoani Simiyu pamoja na kuzindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katika tukio la kipekee linalodhihirisha mapenzi ya wananchi kwa viongozi wao, wakazi wa Mkoa wa Simiyu wamejitokeza kwa wingi kuonyesha furaha na bashasha kuelekea ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kuanza tarehe 15 Juni, 2025.

Wananchi hao wameonyesha utayari wa kumlaki Rais kwa shangwe, huku wakieleza kufurahishwa kwao na hatua mbalimbali za maendeleo zinazoendelea kutekelezwa chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

"Tunampongeza sana Rais wetu Samia, ametuletea maji, umeme na hata barabara ni nzuri," alisema mmoja wa wananchi waliohojiwa na mwandishi wetu, akionesha shukrani kwa mageuzi ya maendeleo yanayoonekana kwa macho.
Ziara hiyo ya kikazi ya Mheshimiwa Rais Samia inatarajiwa kuhusisha uzinduzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati pamoja na kuzungumza na wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha huduma za kijamii na kuinua uchumi wa maeneo ya pembezoni kama Simiyu.

Chanzo: Habari Mpya Tv
 
Hiyo ni danganya toto, barabara bado zina mashimo sehemu nyingi sana hapa Tz, maji pia ni ndoto sehemu kubwa tu, na umeme unakatika kila siku.

Development ya kweli haiko kwenye hotuba, iko kwenye maisha ya watu, na kwa sasa, maisha ni magumu kuliko hata headline ya gazeti.
 
Kwani amesema anakutembelea wewe?
 
Back
Top Bottom