Rais Samia anatekeleza sera za Tundu Lissu?

Rais Samia anatekeleza sera za Tundu Lissu?

malang0

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
440
Reaction score
523
Katika awamu hii mpya ya sita chini ya Rais wetu, Mama Samia tunaona anatekeleza baadhi ya sera za mgombea Urais wa CHADEMA, Mh. Tundu Antipas Lissu. Mojawapo wa sea hizo ni nchi kurudisha diplomasia na nchi za nje na mashirikaya kimataifa kama World Bank IMF, WHO ambazo Mwendazake aliharibu.

Vilevile aligusia TRA kuacha kutoa kodi kwa nguvu na kufungia watu account zao, kuondolewa kwa vitambulisho vya maachinga ambavyo hatujamsikia mama akivisema kabisa tangu aingie madarakani, na kurudisha utawala wa haki na sheria, hizi ni baadhi ya sera Mh. Lissu alikuwa anagipia chapuo kipindi cha kampeni mwaka jana. Je, Rais wetuvanatekeleza sera za CHADEMA?

Nawasalimu kwa jina laJamhuri wa Muungano wa Tanzania.
 
Mwenye kufahamu anakotupeleka Rais Samia Suluhu Hassan naomba atuambie, Kwani ninaona kama vile tunapotea.
 
Mwenye kufahamu anakotupeleka Rais Samia Suluhu Hassan naomba atuambie, Kwani ninaona kama vile tunapotea.
Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Tsh. 2.3391 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Juni 6, 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari siku moja kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Dk Mwigulu amesema mradi iliyopitiwa fedha hizo ni ya uboreshaji wa barabara za vijijini na fursa za kijamii (RISE), mradi wa kuimarisha mazingira ya ufundishaji na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu (Heet).

Miradi mingine ni wa kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za mtandao (DTP) na mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za Umeme Zanzibar (Zesta).

Mwananchi
Hii miradi inayokopewa fedha ni miradi ya Namna gani hii? Mkopo muhimu Ila miradi hii hapana
 
Lissu ana Maono ya mbali sana na anaitakia mema Nchi yetu Tanzania
 
Chochote kizuri chafaa kuiga, ila sii maovu. Uovu yafaa kuuogopa na kuukemea kwa nguvu zote.
 
Siamini hata kidogo kama ndani ya miezi mchache tumeanza kupigishwa kwata na MABEBERU.
Sasa kila kukicha hali inazidi tu kuwa mbaya.
 
Siamini hata kidogo kama ndani ya miezi mchache tumeanza kupigishwa kwata na MABEBERU.
Sasa kila kukicha hali inazidi tu kuwa mbaya.
Unafahamuu mwendazake udongoni alikopa zaidi ya watangulizi wake alikuta deni la nje 45tr akaacha 60 tr?
 
Siamini hata kidogo kama ndani ya miezi mchache tumeanza kupigishwa kwata na MABEBERU.
Sasa kila kukicha hali inazidi tu kuwa mbaya.
Kwa hiyo unakimbizwa na beberu,kwani mtaani kwako hakuna mjumbe wahi fast kukamripoti huyo beberu.
 
Unafahamuu mwendazake udongoni alikopa zaidi ya watangulizi wake alikuta deni la nje 45tr akaacha 60 tr?
Umesahau Kuna riba la Deni hiloo kwamaana ukisema slikopa tril 15 kwa miaka 5 na miezi mitano unamaanisha kila mwaka alikopa tr 3 average. Je liba ya madeni yake iko wa
 
Kuna wakati utafika tutamani nchi iuzwe tulipe madeni kisha pesa itakayosalia tugawane ili kila mmoja akatafute nchi nchi itakayomfaa kuishi! Moyoni nawaza sijui Ubelgiji watanipokea? Ila poa, kazi iendelee, kila nabii na umma wake!
 
Mbona hajasema au kufanya chochote kuhusu ushogeshwaji?
Kwa taarifa yako lisu hakuwa na sera yoyote ya maana na yenye manufaa kwa wananchi au nchi. Ushogeshwaji ndo ilikuwa hoja yake ya msingi aliyolishwa na mabwana zake kuja kutuletea.
 
Back
Top Bottom