Rais Samia anaenda kuweka historia nyingine mpya katika sekta ya elimu licha ya maboresho makubwa yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka 2021/22 kwa sekta ya Elimu, tayari serikali imepanga kutumia kiasi cha takribani Trilioni 2.78 katika miradi ya maendeleo ya Elimu.
pia Kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) serikali imepanga kutumia Trilioni 1.2 ili kuwezesha upatikanaji wa Elimu, ikiwa ni pamoja na mazingira salama ya wasichana kupata elimu.
Vilevile kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) serikali imepanga kutumia Trilioni 1.15 kwaajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na miundombinu katika shule za umma za awali na msingi.
Na mwisho utekelezaji wa program ya Elimu kwa matokeo awamu ya pili (EP4R II) ambapo kiasi cha takribani
Bilioni 435.90 kinalenga kuendeleza ujenzi wa madarasa, vyoo, mabweni na nyumba za walimu.
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inalengo la kupambana na kuuondoa kabisa ujinga ndio maana inawekeza katika elimu