Rais Samia anaweza kutoa mhadhara Chuo kikuu cha Havard au Yale Marekani na dunia nzima ikasimama

sasa mnataka kutupiga, hizo hela za kumpeleka havard nani atalipa? wakina Rafsanjani walitoa mhadhara tukasimamisha masikio walifaidika na nini? Dr Livingstone alitoa mhadhara Edingburg university kuwa kagundua lake akaliita Lake Victoria.
 
Umesifia weee umeona huteuliwi umeamua kumkejeli Mh. Rais sasa. Yule ni mswahili anajua hili ni fumbo na fumbo mfumbie mjinga mwerevu atabaini,sasa hapa umeyatimba siyo kwa kejeli hii.
Endelea na wivu wako.kila mtanzania anafahamu vyema na vizuri sana uwezo mkubwa wa kiakili na upeo alionao Mheshimiwa Rais wetu mpendwa.
 
Unazidi kudhihirisha umbumbumbu wako, aibu kubwa hii unailetea familia yako walahi.
Dah huu nao uchawaaaaaa umezidi
 
sasa mnataka kutupiga, hizo hela za kumpeleka havard nani atalipa? wakina Rafsanjani walitoa mhadhara tukasimamisha masikio walifaidika na nini? Dr Livingstone alitoa mhadhara Edingburg university kuwa kagundua lake akaliita Lake Victoria.
Kwa hiyo wewe hofu yako ni Nauli?
 
Hapo Nkrumah hall tu hana uwezo huo ndio sembuse Marekani?

Labda chuo cha uvuvi Bagamoyo.
 
Mwalimu Nyerere na Mwinyi hawakua wanasoma hotuba zao bali hutoa kichwani, Mkapa alikuwa anasoma alichoandika mwenyewe.
Waliobaki wanaandikiwa kama Jakaya alivyokuwa anaandikiwa na January Makamba kama Samia ataandikiwa na kutumia teleprompter heri hivi hivi sidhani Wamarekani wataelewa hekaya za chura.
 
Rais wetu hategemei kuandikiwa hotuba kwasababu uwezo wake ni mkubwa sana na anaweza kutoa hotuba bila hata kusoma popote pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…