Rais Samia anaweza kutoa mhadhara Chuo kikuu cha Havard au Yale Marekani na dunia nzima ikasimama

Rais Samia anaweza kutoa mhadhara Chuo kikuu cha Havard au Yale Marekani na dunia nzima ikasimama

Mtatufanya tuache kutembelea hili Jukwaa kwasababu ya huu upuuzi wenu mnaotuletea hapa🚮.
Nani alikulazimisha kuingia humu? Mchango gani ulioutoa kuanzisha jukwaa hili? Unatoa shilingi ngapi kwa mwezi kuchangia mishahara ya watumishi wa humu? Ondoka hata dakika hii uone kama jukwaa hili halitaendelea kuwepo ondoka haraka sana humu maana huna faida yoyote ile
 
Nani alikulazimisha kuingia humu? Mchango gani ulioutoa kuanzisha jukwaa hili? Unatoa shilingi ngapi kwa mwezi kuchangia mishahara ya watumishi wa humu? Ondoka hata dakika hii uone kama jukwaa hili halitaendelea kuwepo ondoka haraka sana humu maana huna faida yoyote ile
Hivi kwanini hamuonagi shida kufichua kiwango cha ujinga wenu? 🚮
 
Too much of everything is harmful!!


Umezidi uchawa wakupandishe cheo uwe kunguni kabisa.

JamiiForums acheni kuendekeza upuuzi wa namna hii kama Taifa hautatufikisha popote


Na log out

Maandiko yake yanakupahisia ni mtu mnafiki wa kiasi gani. Hata huyo anayefanyiwa huu unafiki, nina hakika akiona takataka kama hizi, atakuwa anajawa na hasira. Hii ni kumfanya anayefanyiwa unafiki, ni mtu ambaye hana akili.

Ni sawa mtu aje kwangu Bams, aniambie, Bams unajuwa, wewe ndiye mtu tajiri kuliko mtu mwingine yeyote katika bara la Afrika. Kwa vyovyote nitamwona huyo mtu ni mtu mnafiki punguani. Ni nitamchukia kwa kuniona mimi nimekosa akili kiasi cha yeye kuona kuwa naweza kuuamini huo upuuzi wake.

Tumsamehe, hajitambui. Kuna wakati umaskini wa kipato wa kupindukia, husababisha umaskini wa akili, hekima, na reasoning.
 
Maandiko yake yanakupahisia ni mtu mnafiki wa kiasi gani. Hata huyo anayefanyiwa huu unafiki, nina hakika akiona takataka kama hizi, atakuwa anajawa na hasira. Hii ni kumfanya anayefanyiwa unafiki, ni mtu ambaye hana akili.

Ni sawa mtu aje kwangu Bams, aniambie, Bams unajuwa, wewe ndiye mtu tajiri kuliko mtu mwingine yeyote katika bara la Afrika. Kwa vyovyote nitamwona huyo mtu ni mtu mnafiki punguani. Ni nitamchukia kwa kuniona mimi nimekosa akili kiasi cha yeye kuona kuwa naweza kuuamini huo upuuzi wake.

Tumsamehe, hajitambui. Kuna wakati umaskini wa kipato wa kupindukia, husababisha umaskini wa akili, hekima, na reasoning.
Chuki binafsi ndio kitu kinakutesa sana ewe mfuasi wa chama kile kilichopoteza muelekeo na kuendelea kudumaa kila uchwao
 
Ndugu zangu Watanzania,

Chuo kikuu cha Havard kinachopatikana Nchini Marekani ni Chuo Bora kabisa Ulimwenguni ambacho kimekuwa kikishika nafasi ya kwanza kwa Ubora Duniani,huku Yale University nayo ikiwa katika nafasi za juu vilevile, ndipo katika kumi bora unaweza kuona sasa vyuo kama Oxford na Cambridge kutoka Uingereza vikiwemo,japo asilimia na kwa kiasi kikubwa kumi bora hutawaliwa na vyuo vya Marekani tu.

Ni katika vyuo hivyo viwili yaani Havard pamoja na Yale unakuta hata Ma Rais wengi sana walioongoza Taifa la Marekani wametokea na kupita katika vyuo hivyo. Hii ni kwa kuwa vyuo hivyo hubeba na kuchukua vipanga na vijana wenye akili za juu sana na uwezo wa kipekee sana kiakili.tena siyo zile akili za kukariri maandishi na kwenda kuyatema kwenye karatasi ya mtihani bila kuelewa hata maana yake wala umeandika nini.

Ni vyuo vinavyo beba watu wenye akili zinazowaka moto na upeo wa hali ya juu sana .hii ndio sababu vyuo hivi hutoa Na Rais wa Marekani, majasusi na watu mbalimbali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama hususani idara zake za ujasusi na upelelezi yaani CIA au FBI .au kuongoza mabenki na makampuni yao yenye maslahi kwa Taifa lao.hivi ndio vyuo vinatoa watu wenye akili ya kuifanya Marekani kuwa hapo ilipo leo hii.

Nikimuagalia Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, kwa umakini wake, utulivu wake,upeo wake, akili kubwa aliyo nayo kichwani mwake, maarifa na uelewa wa masuala mbalimbali na kujiamini kwake naamini akipata nafasi ya kutoa Mhadhara kwenye vyuo hivyo,kwa hakika Dunia nzima inaweza kusimama na kutetemeka kama tetemeko la ardhi.

Hii ni kwa kuwa Rais Samia ana uwezo mkubwa sana wa kutoa hotuba, kuelezea jambo kwa utulivu, umakini, ufasaha na kwa mpangilio na mtiririko mzuri na wenye kuvutia. Anajuwa kupangilia hotuba katika namna inayoteka hisia za watu na kuvuta wasikilizaji kusikiliza bila kuchoka. Tofauti na mwingine anakuwa anatoa hotuba isiyo na muunganiko wala mtiririko wa kueleweka wala kuvutia.

Mfano jaribu kuangalia na kusoma hotuba za watu kama Dr Martin Luther king Jr hasa hotuba zake za I have a dream, I have been to the mountain top, Beyond Vietnam au Time to break silence, Our God is Marching on, The other American, Three evil of society. Unaweza pia soma hotuba ya Franklin Roosevelt hasa ile wakati anaapishwa, soma pia ya John F Kennedy ya mwaka 1963 kama sijakosea anayosema usiulize Marekani itakufanyia nini bali jiulize utaifanyia nini Marekani. Pia waweza soma ile ya Winston Churchill waziri mkuu wa Uingereza anayosema kuwa watapambana ardhini, angani, majini na popote pale.

Soma pia hotuba ya Barack Obama ile ya 2004 wakati anahutubia mkutano mkuu wa Democrat au ile siku ya kuapishwa au ya kukubali uteuzi au ile ya baada ya kupata ushindi. Waweza pia soma hotuba ya Mwalimu Nyerere ile ya 1995 akiwa mkoani Mbeya uwanja wa Sokoine siku ya wafanyakazi Duniani au ile pale Dodoma juu ya kiongozi aliyekuwa anahitajika kuletwa na wana CCM kwa watanzania kama mgombea au ile ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete siku ya Mazishi ya Hayati Nelson Mandela. Au waweza pia soma Hotuba ya Mama yetu mpendwa siku ameapishwa kuwa Rais wetu, ni hotuba yenye hisia kali sana inayoweza kukububujisha Machozi.

Nawasihi Wafuasi wa CHADEMA wawe wanasoma vitu na mambo mbalimbali ili kuongeza maarifa na uelewa, maana huwa nikiwasikiliza wakizungumza huwa naona aibu sana maana wao wakishindwa hoja na kuishiwa hoja unakuta wanaanza kuporomosha matusi kama vichaa au wendawazimu, mambo ambayo huwezi kuyakuta CCM, ndani ya CCM ni hoja kwa hoja na ndio maana chama kinaendelea kuaminika na kukubalika kwa mamilioni ya watanzania wa rika zote na kuendelea kusalia madarakani.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Anaweza kutoa mhadhara. Ila tunataka kujua utakuwa muhadhara wa nini? Nyie watu, watanzania tunataka maendeleo. Watanzania tunataka uwajibikaji. Watanzania tunataka viongozi waadilifu.
Endeleeni kudanganyana na haya maandishi mengi yasiyo na tija. Muda unakwenda na huwa haurudi nyuma. Mkiendelea kufikiria kila kitu kiko sawa, msilaumu mtu. majuto mjukuu
 
Kama wewe ni akili ndogo huwezi ukaelewa hoja na kuona hoja,ni kwenye afya ya akili ndio anaweza kuelewa nilichokiandika.

Wewe kwa huu upuuzi unaoweka humu, jihesabie ni punguani wa kutupwa. Sasa sijui ni upunguani wa kuzaliwa au uliosababishwa na kukata tamaa ya maisha, yaani yule mtu anayesema nipo tayari kufanya lolote alimradi tu nipate chochote ili niishi.
 
what is economic benefit ya havard presentation, juzi matajiri walikuwa Kigali kwenye africa economic forum and was very successful, hatuhitaji viongozi wetu ku line up europe.

Ruto alienda US muda mchache umepita. And yet, jana amesalimu amri. Serikali iangalie namna ya kupunguza matumizi ili kupunguza ukali wa maisha.
Safari za kwenda kutoa mihadhara ya kukopeshwa na hela zinaishia kwenye matumizi ya kawaida, ni kuwasaliti watu wanaoongozwa.
 
Mimi nipo vizuri na ndio maana nashusha NONDO zinazowatoa jasho.

Wehu wote wanaookota makopo na kusimama katikati ya barabara huwa wanaamini wapo timamu.

Zingatia ushauri wa wanaokuambia uende hospitali. Kijana hupo sawasawa kichwani. Tunaokushauri kwenda hospitali, tunakutakia mema. Hakuna mtu mwenye akili timamu hata mmoja ambaye anaeweza kuudhalilisha utu wake, kama ufanyavyo.
 
Nadhani kwa kuwa Mama yuko humu,tumuombe kama anatusikia akupe kateuzi fulani ili upumue!
 
Back
Top Bottom