Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu ni moja ya viongozi 50 duniani walioalikwa kuhudhuria kongamano la Uchumi duniani linalofanyika nchini Uswisi lakini viongozi kutoka bara la Afrika waliolikwa ni wawili ambao ni yeye na Rais Ramaphosa.
Pamoja na mambo mengine, kongamano la mwaka huu lililoanza Januari 16-20 agenda zake kuu ni mzozo wa Ukraine na Urusi na athari zake mbaya katika nishati na upatikanaji wa chakula duniani.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wafanyabiashara wakubwa ,wanasiasa, watu mashuhuri na wanaharakati wengine.
Kongamano hilo ni fursa kwa Tanzania kwenye uwekezaji hususani katika sekta ya nishati ambayo ni moja ya agenda kuu.
Kutokana na uwekezaji ambao nchi yetu kwa kushirikiana na nchi ya Uganda katika mradi wa Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki(EACOP) inatarajia kufanya ni matumaini yangu Rais Samia atatumia kongamano hilo kushawishi uwekezaji huo.
Kufuatia azimio la bunge la Ulaya lililotolewa mwezi septemba ,2022 la kutaka mradi huo wa EACOP uhairishwe kwa kuwa unakiuka mradi haki za binadamu na athari za mazingira, ninaamini kongamano hilo litakuja na mtazamo mpya.
Kama agenda kuu za kongamano zinavyosema, ni Imani yangu kwamba:
i) Tanzania itanufaika kwa kiasi kikubwa katika uwekezaji wa kilimo ili kuweza kukidhi agenda ya upatikanaji wa chakula
Mpaka sasa mhe. Rais, ameonesha jitihada katika kilimo na katika Mwaka huu wa fedha pekee serikali imetoa kiasi Cha shilingi bilioni 150 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea.
ii) Bomba la mafuta la EACOP litapata uwekezaji ili tatizo la ukosefu wa nishati lipungue na ni matumaini yangu Tanzania itakuwa kitovu Cha uwekezaji katika sekta hii Afrika.
Nauona uchumi wa nchi unavyofunguka kimataifa kupitia uongozi wa Dkt Samia