Rais Samia, anza na Dkt. Abassi ameonesha dharau na kiburi kwako

Rais Samia, anza na Dkt. Abassi ameonesha dharau na kiburi kwako

Na sio kama amefanya kwa bahati mbaya

Anajua ishu zote za protokali

Ukaidi na utovu wa nidhamu
Ukaidi wa hali ya juu na watu wanavyokumbusha angejirudi kidogo lakini ameamua kukomaa
 
Na sio kama amefanya kwa bahati mbaya

Anajua ishu zote za protokali

Ukaidi na utovu wa nidhamu
Ni makosa makubwa sana kuwabakisha hawa masalia kwenye utawala wa mama. Walitakiwa waondoke na yule chogo aliyepelekwa bungeni kwa mlango wa nyuma.
 
sahihi kabisa, yani jamaa ana Access na rais anashindwa kumuuliza kama hajaelewa vizuri anakuja kuropoka kwamba rais hajaongelea magazeti, kwani vyombo vya habari si na magazeti yamo
Hakika
 
Watanzania wamesikia kauli yako ya kutaka vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe ila vifuate sheria

Kama Mkuu wa Nchi na Kama Mama umeona utoe huo msamaha tuanze upya lakini ukasisitiza vifuate Sheria.

Lakini huko kwenye vyombo vya habari kuna ajira nyingi zilipotea na kusimama, amri yako inatoa fursa na ahueni kwenye suala hilo kwani kuna ambao waliathirika kiuchumi kwa kufungiwa huko na kuishi maisha ya tabu

Ila Mama yetu, Katibu Mkuu anayehusika na tasnia ya Habari ameamua kuonesha Kiburi na Jeuri na pia kukosea heshima kwako kama Mkuu wa Nchi kwa kupindisha agizo lako kuwa hukusema vyombo vya habari( hadi magazeti) lakini pia anataka kuonesha kuwa hauwezi kujieleza vizuri ndio maana anasema haukusema na magazeti, alitaka utamke kwa mtiririko kila chombo cha habari ili yeye PhD holder akuelewe.

Yeye ni nani awe na dharau na kiburi namna hii kwa Mkuu wetu wa nchi? Au ni moja ya watu waliokuwa hawataki wewe uwe hapo kwa mawazo yao kuwa hautoweza?

Mama yetu tunajua wewe ni mpole na uliyejaa hekima na busara kutokana kuwa Mama, mzazi, umri na hata asili ya maeneo unayotoka lakini hili lisichukuliwe ni udhaifu( kama ulivyosema kwenye hotuba yako). Inaonekana Dr Abbas anachukulia ni udhaifu na ndio maana ana kiburi cha kupingana na maelekezo yako.

Ni vyema Mama umfanye awe mfano kwa wengine kuwa upole wako na busara sio udhaifu ili wengine wajifunze. Wangoni wanasema "Make a statement"

Cha ajabu pamoja na watu kumkumbusha bado mpaka sasa anaonesha jeuri na kiburi,huyu anakudharau mbele ya macho ya watanzania.

Mama najua una huruma, utu, hekima, upendo kama huwezi kumuweka benchi basi angalia nafasi za maDAS huko mipakani zilizowazi umpangie majukumu mengine

Mama huyu kijana AMEKUZINGUA na wewe MZINGUE
Chochea moto chochea
6ab988fb77c043429002bf86781c90bc.jpg
 
Ili mambo yaende sawa mama anatakiwa ale kichwa
Tena italeta ahueni kuelekea mwanzo mpya katika kuboresha mahusiano ma vyombo vya habari, kubakisha sura ile ile ndio madhara yake haya anakuwa kama anashindana na vyombo vya habari
 
Uvccm wote saizi wamepoteana na kuchanganyukiwa hawaelewi pakuanzia kwa mama
255767980188_status_b9fdd5dd0a5c4857aa99f8ce11732b44.jpg
 
Angetamka Chuma enzi zile asingeleta hizi habari
moja ya mema ya jiwe ni hilo alikuwa akitamka kitu hakuna ubishi au upuuzi. jiwe tutamkumbuka kwa hilo japo nilikuwa simkubali
 
Abbas nia yake ni kutaka kuthibitisha kuwa ile kauli ya "ukinizingua tutazinguana" ilikuwa ya kuchangamsha genge tu wala Mama hana ubavu huo.
 
Katika kuamsha watendaji waliolala either kwa uzembe au kiburi angeanza na huyu mwehu.
 
moja ya mema ya jiwe ni hilo alikuwa akitamka kitu hakuna ubishi au upuuzi. jiwe tutamkumbuka kwa hilo japo nilikuwa simkubali
Uko sahihi, ni vile tu maamuzi mengin hayakuwa sahihi lakini akisema kitu amesem haraka utekelezaji
 
Acha uchochezi usiokuwa na tija, unazani kufunguliwa vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kama kufungua mlango wa choo chako unapobanwa na haja!?
Kwa hiyo unataka kusema rais alikosea kusema vifunguliwe?
 
Dr. Abbas kageuka gumzo mitandaoni, hivi vyombo vya habari kwake yeye sijui ndo online tv tu.
Maana mheshimiwa Rais kashasema vyombo vyote vya habari vifunguliwe.
 
Dr. Abbas kageuka gumzo mitandaoni, hivi vyombo vya habari kwake yeye sijui ndo online tv tu.
Maana mheshimiwa Rais kashasema vyombo vyote vya habari vifunguliwe.
Anajifanya mjuaji
 
Back
Top Bottom