Rais Samia aondoka kwenda Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Yoweri Museveni

Alizikosa sana na sasa ni wakati wake kufanya utalii wa kimataifa
Wakati wa mwendazake mbona alikuwa anasafiri sana, ndio alikuwa anamwakilisha kwenye matukio ya nje ya nchi
 
Tetetetetete
 
Acha mawazo ya kitoto, unataka aende Uganda na bodaboda?. Museveni alikuja kuhudhuria kuapishwa kwa hayati Magufuli, unataka Rais awetu asusie kuapishwa kwake?.
 
Ujinga huu ukiendelea tutarudi nyuma hatua tatu ndo maana tutamkumbuka Sana mwendazke kwani mambo Kama hata alikuwa hayataki kabisa
Mama anapiga misele tu hataki tabu.
Mkwere Og
 
Hizi safari hazina mantiki kwa Tanzania.

Mh Rais hakagui miradi ya SGR, Bwawa la Nyerere, Vituo vya afya, miradi ya maji wala siku hizi hazitangazwi kwenye vyombo vya habari kama ilivyokuwa inafanywa.

"Malkia mwenye maneno matamu..."-TAL
"Mtanikumbuka kwa mambo mazuri sio mabaya..."JPM

Mh Rais atumikie wananchi waliochagua chama chake, ukimya wao asifikiri ni shwari, kutuma wasaidizi wafanye kazi hizo zinamnyima kupigiwa kura kama yeye......huo ndio ukweili unaosemwa chinichini
 
Dah...hizi Safari mnaandika lakini? Maana za JK tulizihesabu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hata hizi zina counter inaendelea na kazi kimyakimya huko, kumbuka hesabu zilisema JK alikuwa ughaibuni kwa 5 years katika uongozi wake wa miaka 10
 
Majaliwa atakuwa anaishia Chato kukagua kaburi. Hakuna kukaimishwa wala kutumwa nje.
 
Siku nilipoona ile twit yake ya "nimewasili dar" nikajua tu kinachofuata, kwa sasa ni kama ame out source majukumu yake
 
Ceremonial President. JK style.
 
Mama mbona hatulii kabisa ofisini hizo per diem watu wanajitafunia tu burebure ili hali kuna wananchi masakini huko dodoma wanakunywa maji yenye tope.

Hakika JPM ataendelea kuishi mioyoni mwa watanzania mengi.
Dodoma wana mbunge wao ambaye ni spika.
Dodoma ni makao makuu ya nchi
 
Airbus tamu tamu sana, hata mkinuna, ni furaha yangu mie....
 
Acha mawazo ya kitoto, unataka aende Uganda na bodaboda?. Museveni alikuja kuhudhuria kuapishwa kwa hayati Magufuli, unataka Rais awetu asusie kuapishwa kwake?.
Kati ya kuapishwa na msiba upi wenye Nguvu? Bakizeni ata akili kidogo mnapompenda mtu maana mmekuwa kama vichaaa
 
Dah...hizi Safari mnaandika lakini? Maana za JK tulizihesabu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Daaaah! Ilikuwa inafurahisha sana! Anastahili pongezi sana aliyeanzisha thread ile!
 
Rais anao wasaidizi wake wanaoendelea na kazi wakati yeye anapohudhuria shughuli ya kuapishwa ya Museveni.

Huwezi kukwepa kushirikiana na jirani yako unayetegemea bomba la mafuta kutoka nchi yake lipitishwe ndani ya nchi yako.

Huwezi kumkwepa Museveni ambaye raia wa Uganda wana muingiliano mkubwa na sisi watanzania.

Hiyo miradi inaweza kukaguliwa na Majaliwa na waziri Kalemani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…