Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Machi, 2025.
View attachment 3262635
Sisi wananchi kama waajiri wao na uwajibikaji kwetu. Ingawa nikili sijui huwa wanajadili nini.
Nilitegemea hawa watu wakitoka hapo kila mmoja aje kwetu kutuambia:
1: Kwa mujibu wa dira ya wizara tuko hapa.
2: Kwa mujibu wa dhima ya wizara tumefikia hapa.
3: Kwa malengo tuliyojiwekea kama wizara tuko pale.
4: Tumefikia malengo kwa kadri tulipo.
5: Hatujafikia malengo kwa hapa tulipo kwa sababu hizi.
6: Mipindi kifuatacho tunaadhimia kufanya hivi na serikali imekubali kuongeza haya ili lile lifanyike au imekubali kuondoa hiki na kile.
7: Tutarajie haya ambayo tutayapima kikao kijacho, nikiwa na mrejesho wake.
Kwetu ni kimya kimya, kama bosi malengo yake hayajulikani, je wa chini yake anatengeneza malengo na kufanyiwa tathmini toka wapi na kwa jinsi gani?
Waziri anatoka hapo anaenda kufunga msuli ili kufatilia na kufanya utekelezaji zaidi maana kikao kijacho atatakiwa kuonyesha uwajibikaji.
Au hata kuwa na mazungumzo ya wazi na waandishi wa habari na wananchi kuhusiana na kazi za wizara zao. Ingawa waandishi wasiwe wa kuteuliwa au maelekezo maalumu.
Nawaza tu kwa kuandika.