Katika hatua ya fainali mechi mtakayoshinda, goli moja, goli la mama ni shilingi milioni 30” maneno ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitangaza dau jipya ambalo mnyama atajinyakulia katika kila goli watakalofunga kwenye mechi ambayo wao wataibuka washindi.
Soma Pia: Rais Samia apandisha dau 'Goli la Mama' kwa Simba SC, kila Goli TSh. milioni 10 kwa mchezo wa CAF
Ni kwenye safari yake ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC). Mechi ya mkondo wa kwanza ya fainali itapigwa Mei 17 nchini Morocco na mkondo wa pili ni Mei 25, Tanzani.