SI KWELI Rais Samia apiga picha na bango likiwa na maneno 'naogopa uchaguzi naomba watanzania mniteue'

SI KWELI Rais Samia apiga picha na bango likiwa na maneno 'naogopa uchaguzi naomba watanzania mniteue'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
PICHA SAMIA.jpg
 
Tunachokijua
Samia Suluhu Hassan ni Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliapishwa Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Rais Samia ni mwanamke wa kwanza nchini kushika nafasi za Makamu wa Rais na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 Chama cha mapinduzi kupitia mkutano mkuu uliofanyika jijini Dodoma kilimteua rasmi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu kupitia tiketi ya chama hicho.

Kumekuwapo na picha inayosambaa mtandao ikionesha picha ya Rais Samia akiwa ameshika picha ikiwa na maneno 'naogopa uchaguzi naomba watanzania mniteue'


Je, uhalisia wa picha hiyo ni upi?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa picha hiyo si halisi bali ilitengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba (AI)

Aidha picha hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambayo yanaithibitisha kuwa imetengenezwa kwa akili mnemba, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutokuwepo kwa mishikio ya miwani ambayo husaidia katika uvaaji wa miwani, uwepo wa bendera inayoonekana kuwa ya Tanzania upande wa nyuma lakini mpangilio wa rangi za bendera hiyo si sahihi huku rangi ya kijani inayotambulisha uoto wa asili ikikosekana badala yake ikiwekwa bluu. Kimo cha mlingoti wa bendera kisicho cha kawaida.

Vilevile kifaa cha utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia akili mnemba kinaainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa teknolojia hiyo kwa asilimia 99%
screenshot-2025-02-11-091735-png.3232893


Hata hivyo hivi karibuni kumekuwapo na maudhui mengi ya picha na video kumhusu Rais Samia yakiwa yametengenezwa kwa akili mnemba hivyo ni vema kupata maarifa ya namna ya kutambua maudhui hayo ili kuepuka taharuki zinazoweza kutokana na maudhui husika.​
Sio yeye tuma picha ile ambayo inaelezea kuwa piga simu
 
Hayo madole yameshika picha pia sio ya kipemba.Hizo ndole za ......
 
Back
Top Bottom