Rais Samia Apongeza Juhudi za Kampuni ya Bia ya Serengeti katika Utunzaji wa Mazingira

Rais Samia Apongeza Juhudi za Kampuni ya Bia ya Serengeti katika Utunzaji wa Mazingira

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
721
Reaction score
438



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,ametoa tuzo kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa kampuni na wadau wengine katika juhudi zao za uhifadhi wa mazingira na kuliletea taifa maendeleo endelevu.

Tuzo hiyo ya kihistoria Pongezi ambao ni ya kwanza kwa SBL kutolewa na kingozi mkuu wa nchi, zinaonesha dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika utekelezaji wa mipango ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG).


Kupitia programu zake mbalimbali, SBL hadi sasa imefanikiwa:

● Kupanda miti zaidi ya 10,000 katika Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati

● Kutekeleza miradi ya maji safi na salama zaidi ya 28 kwa jamii zinazozunguka maeneo yake ya uzalishaji

● Kuwekeza katika kilimo endelevu kwa kuunga mkono vijana zaidi ya 300 kupitia mpango wa Kilimo Viwanda

Aidha, SBL imeanzisha mpango wa Shamba ni Mali, unaolenga kuwapatia wakulima mbolea, mbegu bora, teknolojia ya kisasa na elimu ya kilimo, na lengo la kuwafikia wakulima zaidi ya 4,000 ifikapo mwaka 2030.

Utambuzi huu unaakisi mchango wa SBL kama mdau anayejali mazingira na kuthamini jamii anazozihudumia, sambamba na kuunga mkono ajenda ya Taifa ya maendeleo endelevu.
​
 
Kitu gani? Nchi hii si tumekubaliana haina dini? Sasa kila muislam atachagua mwenyewe, dunia au akhera
Uache kujifanya kutoa ushauri kwa viongozi wa CHADEMA kama unalijua hilo.
 
Back
Top Bottom