Rais Samia apongezwa Bungeni kwa kuwajali vijana

Rais Samia apongezwa Bungeni kwa kuwajali vijana

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mbunge wa Viti Maalum, Ngw'asi Kamani amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali vijana na kuondoa malipo ya kodi ya mwaka mmoja wanapoanza biashara.

Akichangia bungeni Aprili 11, 2023 katika mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2023/24, Kamani alimshukuru Rais kwa kuondoa malipo hayo kwa kuwa kwa muda mrefu vijana walikuwa wakilalamika wanapoanzisha biashara kunakuwa na mlolongo wa taratibu na urasimu kabla ya kusimama kwenye biashara zao.

"Tangu Rais alipoingia madarakani amehakikisha anatulea sisi vijana na ku-tuaminisha kuwa tuna mtu anatuunga mkono katika kujenga taifa letu," alisema Kamani.

Pia alishauri serikali iwasilishe bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ili kukuza uwazi kwenye utumishi wa umma na kuchochea uzalendo kwa vijana.
 
Back
Top Bottom