Rais Samia ashiriki Hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa Block Farming, Dodoma - Machi 20, 2023

Kwahiyo unajaribu kusema nini!,mradi hauna tija? wewe kama hauna muitikio na kujitambua Wacha wengine wafanye ukizinduka wenzako wanarauka . Baki apo kulaumu kama mgema madafu
 
Another scenario, kwakua small holder farmers ni wengi kuliko hawa wapya costs of production kwenye hizo blocks definately zitakuwa kubwa kuliko wao wasiozingatia management of their farms so ni soko lipi ambalo litanunua products zao ambazo zita compete kwenye bei na hawa ambao hawana standards wala hawaweki enough efforts kwenye productions zao? Utatumia serikali kama market maana watakuwa protected in the first yeara ili project ionekane kuwa ni viable what will be the effect kwa market ya locals? Je wakikosa soko kwa mazao yao serikali itafanyaje maana cash ndiyo inapatikana kwenye kilimo as the only means of livelihoods kwa hao rural population ambayo ndiyo true voters
 
Kwahiyo unajaribu kusema nini!,mradi hauna tija? wewe kama hauna muitikio na kujitambua Wacha wengine wafanye ukizinduka wenzako wanarauka . Baki apo kulaumu kama mgema madafu
Najaribu kusema tuache siasa kwanza tusaidie technicalities siasa itakuja kama secondary criteria na siyo primary kwakua bado hizi ni first phase trials at national level...Tuache ushabiki kama tunataka kuisaidia nchi
 
dodoma ni sehemu kame ambayo hata uzalishaji wa mazao ya vyakula ni mgumu lkn cha ajabu ati ndo unakuwa pilot region badala ya mikoa ya mbeya,ruvuma,rukwa,katavi nk.mikoa ambayo wananchi wake ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya vyakula hapa nchini.dododma maji ni ya shida na sijui ni nani aliyependekeza project hiyo ianzie huko.kwa haraka haraka utaona jinsi gani viongozi wetu wanavyoyapeleka mambo kisiasa.project kama hiyo niliwahi kuikuta pale kigoma sehemu moja inayoitwa kazegunga nje kidogo kigoma mjini lkn kwa bahati mbaya haikuzaa matunda na kwa sasa ukienda pale yale mashamba ya block farming yamezalisha mji mkubwa wa kisasa.
sehemu ile iko karibu sana na bonde la maji yanayotiririka karibu kwa kipindi cha mwaka mzima liitwalo bonde la mungonya.sasa najaribu kuwaza huko dodoma tena chinangali ambapo ni pakame kabisa je kweli patakuwa na tija yoyote?Tuombe Mungu itokee muijiza.
 
Water basin ni kubwa sana Dodoma, na maji mengine for irritation schemes yanaweza patikana kwenye Man made dams kubwa kubwa na kuvuna maji ya mvua for all season ya kilimo na pia waki drill maji mengi sana Dodoma. Acha kuwa short sighted, myopic..!!
its a daylight dreams.
 
Hapana, hao wahusika watapatiwa mafunzo kwanza ya miezi mitatu, kisha baada ya hapo ndio wataingia shambani, watu hawaokotwi mtaani kama ulivyoandika.
 
Kwahiyo unajaribu kusema nini!,mradi hauna tija? wewe kama hauna muitikio na kujitambua Wacha wengine wafanye ukizinduka wenzako wanarauka . Baki apo kulaumu kama mgema madafu
Aise, mbona una panic? Hii tu inakuondoa kwenye kutaka kuelewa badala yake unakuwa defensive...
 
I think Dodoma kwa zao la zabibu is a perfect site...Tatizo ni misingi iliyowekwa ni dhaifu kiutaalam na aliye design ni mwanasiasa ambaye analenga kura zaidi kuliko kuangalia welfare ya watanzania kwa ujumla...Si vibaya, lakini kinachosikitisha ni Rais ndiye atakuwa victim baadaye hata baada ya kupata hizo kura na Rais anayekuja baada ya yeye ndiye atatakiwa kuanza kumsema vibaya kwakua atakuwa hana choice...It is also whats happening now kwa JPM...Mnapanga mipango siyo sustainable yenye boom ambayo ina burst baadaye na kutafuta bangusilo....

Strategists wetu ni wazuri kwenye siasa maana wana trainings nzuri za kisiasa lakini wana udhaifu kwenye interdisciplinarity na hata kwenye political economy...Kisha mbinu zao nyingi ni za kibabe i.e command and control na siyo zenye economic incentives...Ni Institution ilivyo evolve over time.

Wanapopatiwa critics wana resort kwenye defence badala ya kuwa na uwezo wa kupokea feedbacks ambazo zitawajenga zaidi

Kinachotokea kenya sasa hivi ni exactly kitakachokuja kutokea baadaye Tanzania....It means kama Rais atashinda 2025, then 2030 atakapokuwa anaondoka atakuwa the least popular kwakua ajira bado litakuwa tatizo la uhalisia tena zaidi ya sasa...Maana msingi unaojengwa nikutoa expectations kwamba vijana wanapatiwa ajita binafsi wakati kiuhalisia mbinu hii haiwezi ku absorb vijana wengi na kwakua land ni limited itakwama mapema sana huku baadaye ikiwa haipo namna ya ku absotbe hao wengine na hawa kama itakuwa vipi watakuwa wameshaonyesha ku fail wengi wao na pengine kuenda kwenye easy options kuliko ya kilimo kwasababu ya factors ambazo kwa sasa wamezi assume kama constant...
 
Nimemsikia mtangazaji mmoja anasema BBTT ameitamka Bibi Titi
 
Best of luck
 
A

Hapachezwi kamari hapo hata pategemewe "lady luck".

Serikali inayorndeshwa na mama Samia imetowa fursa kwa vitendo. Vijana muweze au mshindwe kuitumia fursa hiyo ni juu yenu.
Mradi mipango ni thabiti na kuna mnunuzi atakaepewa block kubwa zaidi sasa shida itoke wapi na vijana wanapewa training what to worry.

Kumbuka tu sio kila mtu ‘Unilever’ usije kwenda Mfindi ukaona mashamba ya chai yanapouza kwa mtu mmoja ukadhani kila mkulima ni sawa nao.

Unilever ni conglomerate kwenye ‘fast moving consumer goods’ ulimwenguni so ana kila interest ya kusaidia ata wakulima wadogo alipo maana wao wana access ya soko kubwa sana duniani la chai na wanamiliki brand kibao tofauti za chai tu, achilia vitu vingine.

Ni hivi mimi nimemsikiliza Bashe and you don’t want my take on this trust me, so tuachie hapo kwenye all the best.
 
Reactions: Ame
Kijana hujausoma mradi wala hujauelewa, unapeleka fikra zako kwa yasiyokuwepo.

Usome kisha urudi na uelewa. Kama huwezi kuusoma mradi basi japo itazame video ya uzinduzi utapata idea ya mradi na utakuja na vitu vyenye mashiko (relevant).

Usiwe mvivu kusoma.
 
We kama umeulewa masoko ya hao wakulima wadogo ni nani?
 
Binafsi naamini mpaka huu mradi umetengewa fedha nyingi lazima tayari masoko ya nje yamekwisha andaliwa ya ndani na nje ya Africa na mradi utafaulu kwa kiwango kikubwa sana tuache kubeza jitihada nzuri kama hizi.

Huu mradi haupo kabisa kisiasa bali katika kuhakikisha sekta ya Kilimo cha mazao kinaongeza pato la taifa.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Hiyo program imeratibiwa Kwa Kila kitu, unadhani wanaolima kienyeji kama huko mtaani kwenu?

Wanaolima mazao elekezi yenye soko kabisa sio tuu ndani Bali masoko ya Nje ambayo serikali imewatafitia.
Kiongozi watu ni wavivu WA kuelewa mbona WAZIRI ameeleza kila hatua ya huu mradi mpaka masoko watakavyouza? watu wanakalia ubishi hawataki kufuatilia mpango mkakati WA selikari katika kuliendea jambo hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…