Rais Samia ashiriki Kikao na Maafisa Ugani, Ikulu ya Chamwino, Agosti 10, 2024

Rais Samia ashiriki Kikao na Maafisa Ugani, Ikulu ya Chamwino, Agosti 10, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Akishiriki Kikao na Maafisa Ugani na Wanaushirika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 10 Agosti, 2024.

1723297381785.jpeg

UPDATES

ABDULMAJID NSEKELA, M/kiti Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika

Vyama vya ushirika nchini vipo 7612, hadi sasa vyama 6350 vimeshasajiliwa katika mfumo muhimu mpya wa MOVE kupitia Wizara. Kusajili vyama hivyo ni moja, lakini kuhakikisha wakulima wote wanasajiliwa ni muhimu. Kwa wakulima zaidi ya milioni 8 hadi sasa wakulima milioni 1.2 wameshaandikishwa katika mfumo wa MOVE.

Hii inaleta tija katika maana ya data, uhudumiaji lakini takwimu njema za kujenga sera za kuhudumia.

Mh. Rais, eneo la tatu ambalo tulilizingatia ni kuhakikisha, ushirika umekuwa na sheria nyingi kwa muda mrefu na Mh. Rais umekuwa ukisema sheria kinzani ziangaliwe. Jambo la kwanza ilikuwa ni kuangalia sera balimbali za ushirika na kutoa mapendekezo ambayo tumeshapeleka draft wizarani na kamati yetu ya bunge wanaziangalia. Hizi zitaleta ushirika wa kisasa ambao tunataka kuuona.

Eneo lingine ni kuangalia mali za ushirika. Wana mali nyingi ambazo aidha hawazifahamu au hazipo katika vitabu halisia. Na lilikuwa ni ombi mojawapo la Mh. Waziri. Kazi hii imeendelea, nah ii inaendana na reforms ambapo hadi sasa, vyama 610 vimeshakaguliwa kwa mali zake zote hadi sasa vyenye thamani ya 4.2 trilioni. Vimeshatambuliwa na kuingizwa katika mfumo sahihi.

Pia soma: Rais Samia awaagiza Wizara ya Utamaduni kuwafundisha vijana mila na desturi kupitia michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA

Mh. Rais, unaweza kuona kama vyama 610 vina thamani ya trilioni 4.2, ni kiasi gani itakuwa tutakapofika 7600.

Mh. Rais, eneo lingine lililo la msingi tuliangalia ushirika lazima ufanye kazi na wadau. Tukasema kwamba wapo wadau wengi sana nchini wanajishughulisha na mambo ya ushirika lakini shughuli zao hazijaunganishwa katika mnyororo wa ufanyaji kazi ili kuleta ushirikiano. Kwahiyo tuliitisha wadau wote nchini na tukawafanyia mapping na tuka-link na zao husika ili waanze kufanya kazi pamoja.

Lakini jambo linjgine ni kuwa kuna wadau wa ushirika ambao wapo nje ya nchi. Kutokana na uzoefu huo, tukashirikiana nao na mpaka sasa tupo nao kuendelea kujadiliana kutengeneza muundo wa kisasa utakaoleta mabadiliko katika ushirika pamoja na kujengea uwezo, kwa maana kwamba wanaushirika wengi wapo vijijini.

Washirika wapo vijijini, wana fedha nyingi ambazo wanatunza ndani ya nyumba zao, tukaja na wazo la kuanzisha benki ya ushirika nchini kwa kuunganisha benki ya KCBL...

Tukasema ili benki ifanye fizuri, wanaushirika lazima watengewe asilimia 51 kama wamiliki waanze kununua hisa. Tunafahamu malengo yetu ilikuwa ni kupata mtaji wa bilioni 20, ingawa kisheria bilioni 15 zinaweza kutosha kuanzisha benki. Lakini ili tuanze vizuri, tulijiwekea malengo ya bilioni 20. Mh. Rais, hadi sasa tumeshapata bilioni 16.9 ya kuanzisha benki hiyo.

Lakini jambo lingine muhimu, tumeshafanya taratibu zinazotakiwa na tumeshapata leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kazi nzuri na sapoti waliotupa, Mh. Rais.

HUSSEIN BASHE, Waziri wa Kilimo
Wakati unaingia madarakani Mh. Rais, bajeti kwa ajili ya ugani ilikuwa ni shilingi milioni 682 mwaka 2021, baadaye ukaiongeza mpaka bilioni 17.7. Mwaka huu wa fedha wa 2024/25. Sasa hizi fedha zianaenda wapi?

Umenunua pikipiki 6439 kwa ajili ya mafias kilimo wan chi hii. Na za mwizo umezikabidhi juzi hivyo pikipiki sasa kufikia jumla ya 6800 kwaajili ya maafuza kilimo. Tutakuwa tumemaliza suala la maafisa kilimo kuwa na vitendeakazi. Mheshimiwa Rais hukuishia hapo, ukatoa fedha. Hivi sasa tumenunua jumla ya magari 46. Lengo ni kwamba kila idara, kwa kuwa kmaafisa ugani tayari wana pikipiki, anayefuata hapa kwenye shughuli za usimamizi wa kilimo ni afisa kilimo.

SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Tanzania
Rais Samia amesema Serikali ina dhamira ya kurudisha hadhi ya ushirika hususan ushirika wa mazao hivyo ametaka Ushirika uendeshwe kisasa, uwekezaji ufanywe kitaalam na ukiwa na lengo la kumnufaisha mwanaushirika moja kwa moja.

Amevitaka Vyama vya Ushirika kutokuwa sehemu ya kumyonya mwana ushirika, bali viwe mstari wa mbele kuwalinda na kuwatetea.

Amevielekeza Vyama vya Ushirika kuwa chachu ya mabadiliko na vyenye kuleta mageuzi ya fikra, ikiwemo kuchangia maendeleo mapana kwa kuhamasisha wanaushirika waweze kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote.

Ameagiza Maafisa Ugani na Maafisa Ushirika kuhakikisha kuwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa na Serikali inaleta matokeo makubwa zaidi, kuwafikia wananchi vijijini pamoja na kuwaelimisha mbinu bora za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Ameitaka Wizara ya Kilimo kuandaa utaratibu wa kuwapima Maafisa Ugani kwa tija inayozalishwa kwenye Kata au Kijiji anachokisimamia ili uwekezaji unaoufanywa na Serikali utoe matokeo yanayotarajiwa.

Amewataka Maafisa Ugani katika ngazi ya Kata kukaa kwenye vituo vyao na kutumia usafiri ambao Serikali imewapatia kuwafikia na kuwahudumia wananchi.

Ameeleza kuwa Serikali itaunga mkono juhudi za wanaushirika kuanzisha Benki ya Ushirika ya Taifa kwa kuchangia Shilingi Bilioni 5 kama mtaji ili kuwezesha shughuli za Benki hiyo kuanza.
 
Nimefurahi kumsikia akilisemea na kulitambua kundi la wananchi wanyonge. Ni wakati sasa wa kupunguza ziara za nje ya nchi ili kubana matumizi ya serikali. Na pia kudhibiti mfumko wa bei
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na maafisa ugani na wanaushirika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma, tarehe 10 Agosti, 2024.
 

Attachments

  • IMG-20240810-WA0191.jpg
    IMG-20240810-WA0191.jpg
    71 KB · Views: 5
  • IMG-20240810-WA0190.jpg
    IMG-20240810-WA0190.jpg
    96.2 KB · Views: 5
  • IMG-20240810-WA0189.jpg
    IMG-20240810-WA0189.jpg
    102.1 KB · Views: 5
  • IMG-20240810-WA0188.jpg
    IMG-20240810-WA0188.jpg
    102.8 KB · Views: 5
  • IMG-20240810-WA0187.jpg
    IMG-20240810-WA0187.jpg
    39.1 KB · Views: 4
  • IMG-20240810-WA0186.jpg
    IMG-20240810-WA0186.jpg
    41.5 KB · Views: 5
Back
Top Bottom