Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan licha ya jana kushinda kutwa nzima akifanya kazi mbalimbali pasipo kupumzika .
lakini leo hii asubuhi na Mapema amewahi sana kuhudhuria misa takatifu ya Kumbukizi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika kanisa la mtakatifu Francis Xaviel Nyakahoja Mkoani Mwanza.
Ndio maana tunasema kuwa Rais wetu amejitoa na kujitolea Maisha yake kwa ajili ya kuwatumikia watanzania na kugusa maisha ya watanzania,kuleta tabasamu na matumaini kwenye mioyo ya watanzania.
Embu fikiria ndugu yangu pamoja na majukumu mazito aliyoyafanya Mama yetu siku ya jana lakini leo anakuwa wakwanza kuamka na kwenda kanisani kuungana na waumini wengine katika misa takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa. Hii maana yake ni kuwa tuna Rais na kiongozi ambaye yupo kazini muda wote,tuna Rais mwenye nguvu na uwezo wa kufanya kazi muda wote.
Tuna Rais na kiongozi mwenye utayari na Pumzi ya kufanya kazi muda wote na saa yoyote ile.wakati muda huu kuna wengine hawajaamka na wengine pengine bado hawajafika makazini kwao .lakini Mama yetu Mpendwa ameamka mapema sana mpaka kufika kanisani.
Hii maana yake mawazo na akili ya Mama yetu na RAIS wetu ipo kwa watanzania na Taifa letu.ndio maana pamoja na cheo chake kikubwa hataki kulala muda wote au kustarehe tu.yeye muda wote yupo na watanzania.hii ndio sababu siku zote anasema kuwa yeye ni mtumishi wa watanzania wote na yupo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.