Rais Samia ashiriki Mkutano wa pamoja kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa pamoja kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani ambapo amesema kwa sasa kiwango cha Biashara ni kidogo kulinganisha na fursa zilizopo

Amesema angependa kuona Biashara inaongezeka kwani Tanzania ni mwanachama wa SADC na EAC ambazo zinatoa fursa za Wawekezaji na Wafanyabiashara kwa soko la Watu Milioni 450, hivyo kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji

Amehimiza kuimarishwa Biashara kwa Nchi hizo mbili ili kuwepo faida kwa pande zote

 
Bila uwepo wa uongozi bora unao zingatia misingi ya sheria ni ngumu sana kufikia malengo anayo waza kwa maendeleo ya taifa.
 
Biashara bongo??
1.Umeme hautoshi
2. Kodi ziko juu,
3.Mafuta juu
4. Ukiritimba
5. Rushwa
6. Ugaidi
 
Akitoka amerika sijui ataenda taifa gani
 
H
Hongera afanye juu chini tupate wawekezaji
 
Ni muwekezaji mwendawazimu peke yake anayeweza kuwekeza Tanzania, we nchi hata wasomali imewashinda kufanya bisahara nani aje. Maana mkiishiwa tu mnaanza kufungia akaunti zao na kuchukua hela. No strategy no use of brain and academia simply siasa za majitaka na mihemko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…