Rais Samia ashuhudia utiaji saini Ujenzi wa SGR kipande cha Nne (Tabora - Isaka 165km), aeleza kutoridhishwa na utendaji wa TPA

Mbona bandari ya Dar huonekana mabehewa ya Uganda Railway ya kubeba mizigo!
 
Kuna kitu hakiko sawa kabisa Nchini kwetu hapa, kuna miradi inafanyika bila kufanya tathimini ya kina na mwisho wa siku inakuwa white elephant. Tuwe wakweli Bandari yetu inapokea mizigo mingi ya DRC na Burundi. Halafu leo hii badala upeleke reli Kigoma ambapo utatrap soko ya DRC na Burundi unapeleka Isaka unamupelekea nani?
 
Kauli zake za kuwapa kipau mbele sekta binafsi ajue sekta binafsi yetu imejaa wahuni wala hawakidhi sifa. Wengi ni wababaishaji wanaotaka kudandia mtaji wa serikali na kupora kutoka umma badala ya kuwekeza mtaji wao.

Samia awe macho na wababaishaji wenyeji. Bora kuleta wawekezaji wa nje wa kweli, yaani wana mtaji kuliko wababaishaji wa ndani. Hao watavuruga badala ya kupata matokeo yaliyotarajiwa wataibia umma.
 
Mimi katika tembeatembea zangu nimeona SGR inakimbilia Tabora ila hiyo ya Kigoma Gitega kupasua hiyo Milima itachukua muda mtefu sana na hienda isiwe na faida.
 
Tunataka barabara kwanza, hizo siasa zenu za reli zitafuata mkituletea barabara maana ma reli yenu hayasaidii kutoa Mazao yangu kijijini.
 
Hongera zake. Kila siku anatia tu saini! Kipande cha kutoka Dar Moro, mwaka wa 2 huu, ni sound tu.

Mara treni itaanza rasmi safari zake mwezi fulani! Ukifika huo mwezi wanasogeza tena!
Aliyekaa nayo miaka 6 kila siku reli reli na hakumaliza utiaji saini vipande vingine je?
 
Watanzania tunaona kazi kubwa anayo ifanya Rais wetu, tupo pamoja naye kila hatua, jukumu letu kubwa ni kutekeleza yale yote anayo yaelekeza haswa kwa watendaji.

watendaji tuache uzembe, kuanzia sasa mtendaji yeyote atakaye zembea kutimiza wajibu wake tutamchukulia kama anahujumu jitihada za Rais.
 
Kipande cha kutokea Morogoro mpaka Makutupora kimefikia asilimia ngapi za ujenzi wake?
Kadogosa kasema hapo juu "asili mia 87", sijui kama ni kweli.
Kama ni kweli, hiyo ni hatua nzuri.
 
Ingawa urais ni taasisi lakini lazima apatikane mtu mwenye weledi wa kusimamia hiyo taasisi iwe imara.
 
Ingawa urais ni taasisi lakini lazima apatikane mtu mwenye weledi wa kusimamia hiyo taasisi iwe imara.
Sio lazima,weledi wa kuua Wananchi na kuwapoteza, Weledi wa kuwafanya Wapinzani Watanzania wenzako kuwa Maadui wa Taifa.

Taasisi iwe imara tu.
 
We jamaa FALAsi kweli
Msamehe hajui umuhimu wa reli huyo ni chawa pro hata aambiwe avue nguo atembee uchi hawezi kataa.

Watu wenye akili wanawekeza kwenye ujenzi wa reli...aende akasome hii The Yiwu-Madrid railway.


#MaendeleoHayanaChama
 

Rais Samia ashuhudia utiaji saini Ujenzi wa SGR kipande cha Nne (Tabora - Isaka 165km ikulu badala ya kufika Tabora kwenye eneo la mradi?​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…