G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Kama kuna mtu anadhani kuwa kwa sababu tu Rais Samia ni mama basi atahurumiwa pale anapovurunda kutokana na jinsia yake basi anajidanganya.
Siasa ni ngumu na unatakiwa kuwa himilivu kweli kweli. Ukitaka kujua hilo angalia siasa za wenzetu kama Kenya ama Marekani. Kiongozi anaangaliwa kama kiongozi na siyo jinsia yake.
Watanzania neno kunyoa tu nanga zimewapaa wakati safari bado ni ndefu. Hilo ni neno la kawaida sana kwenye siasa. Nimeanza kuamini kuwa watanzania wengi ni watu wa huruma huruma sana. Mama kusemwa kuwa atanyolewa basi imekuwa tabu kweli kweli.
Yani inawezekana hata siku akivurunda kisha akaja mbele yetu akalia tutaishia kumuomba sisi msamaha (?) Emb mufike mahali mbadilike maana mnakuwa nyuma mno kwenye vilinge vya siasa.
Tujiandae kukutana na kauli nzito nzito zaidi ya kijikauli chepesi sana cha Mdude Nyangali. Kumbukeni kuwa serikali iliyomshughulikia Mdude na Lissu basi Samia alikuwemo ndani. Usitarajie maneno mepesi tena kwa mtu aliyepotezewa malengo na muda kwa zaidi ya mwaka.
Hivi ni nani kati yenu akicheleweshewa tu mshahara wake anakuwa na furaha kwa boss wake? Sembuse kufungwa? Kumiminiwa risasi? Ukiwa unawalaumu hawa watu jichunguze kwanza ni jambo gani kubwa amewahi kukufanyia mwenzako kwa ubaya na jinsi ulivyomkasirikia? Halafu linganisha na lililowakuta hawa. Unajua ni kitu gani Chadema walifanyiwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita? Bado unataka wawe soft soft?
Emb jiangalieni bwana. Mama kama mnataka kumsaidia mwambieni ahimarishe mifumo ikiwemo katiba yenye meno na inayoeleweka. Vinginevyo basi jiandaeni kuwa kina watu wa huruma sana. Mnakera eti mama mama mama!