kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Wakati wa awamu ya Mzee Mwinyi tukitoka kwenye mfumo wa dola kama ndio engine ya uchumi tulifungua milango na madirisha kwa wawekezaji. Waliingia wababaishaji na matapeli wa kila aina wakijifanya wawekezaji na kusababisha uharibifu wa uchumi wetu. Mzee Mwinyi kwa uungwana wake alikiri makosa baada ya kumaliza awamu yake akidai ukifungua milango upepo mzuri nzi na mbu pia wanaingia.
Katika awamu ya mkapa nzi na mbu wamesumbua vilivyo kwa kuvuruga mpango wa kubinafsisha viwanda. Ama walivipata viwanda kwa bei che na kuviua kuhakikisha masoko kwa viwanda vyao nje ama kuvigeuza kua bohari kwa biashara zao zingine. Asilimia chini ya 10 ndio viwanda vilivyoendelezwa kwa ufanisi.
Tunachotaka kwa Mama Samia sio lugha ya udhaifu kwa wawekezaji au kuwatangazia shamba la kuvuna bure. Tunajua wawekezaji wanatuhitaji kuliko tunavyowahitaji. Hatutaki uwekezaji mradi uwekezaji. Uwekezaji lazima uambatane na manufaa stahiki. Hatutaki bora uwekezaji tunataka uwekezaji bora.
Samia asije fanya makosa kwa legacy ya JPM. Tutarudi hukohuko kwenye rushwa na ufisadi.
Mama take care ccm isije kukufia mikononi maana ile asilimia 84.5 ya kura za Magufuli ni tamko la Watanzania.