Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini mkubwa na kufanya tathmini ya hali ya utendaji wa kazi wa watumishi wa serikali katika mikoa ya Tabora, Arusha na Dar es salaam ambapo mitandao ya kijamii inaonyesha namna wakuu wa mikoa wanavyotekeleza majukumu yao ya usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za serikali.
Ikumbukwe kuwa hawa ni wateule wa Rais na ndio waliopewa dhamana ya kushughulika na maendeleo ndani ya mikoa yao.
Jana nimeona watu wakilaumu Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za kinidhamu kwa wakuu wa Idara waliokaa muda mrefu katika Halmashauri huku wengine wakidai hana mamlaka hayo, leo nataka nitoe somo ili wale wote mnaotaka kujua mamlaka ya wakuu wa mikoa msome na kuelewa mamlaka ya Mkuu wa Mkoa katika kushughulika na watumishi wazembe kama kule Arusha.
Wengi wasiojua nataka niwape elimu ili mjue kuanzia leo Mkuu wa Mkoa anapata wapi mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi.
Mkuu wa Mkoa ana mamlaka Kikatiba, ana Mamlaka kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009 na ana mamlaka pia kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa Na.19 ya Mwaka 1997.
Kikatiba, Ibara ya 61 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa kila Mkuu wa Mkoa atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za serikali ya Jamhuri ya Muungano katika Mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria au kwa mujibu wa sheria kama ni kazi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge." mwisho wa kunukuu.
Kwa maana hiyo Sheria za Utumishi wa Umma Na 08 za mwaka 2002 zilizotungwa na Bunge RC ana ana mamlaka nazo.Katiba imempa mamlaka kushughulika na jambo lolote ambalo bunge imelitungia sheria.Mkuu wa Mkoa anakuwa hatendi haki kama wananchi wanalalamikia hawapati maji, umeme, barabara, ardhi, mifugo, pembejeo na yeye anapuuzia.
Mkuu wa Mkoa hawezi kukaa kimya wakati thamani ya miradi haiendani na fedha zilizotolewa, Mkuu wa Mkoa hawezi kukaa kimya kwa kuogopa kuchukua hatua pindi haki za wananchi zinapodhulumiwa.Aliyempa kazi amemtaka akatatue kero za wananchi na kweli Makonda ameonekana kuwa na mvuto mno.Mikoa yote wananchi wake wanafuatilia mikutano yake mwanaume huyu wa shoka.
Pili, Mkuu wa Mkoa ametajwa katika Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009 kanuni B.15 ambayo nainukuu, " (1) The Regional Commissioner or District Commissioner is the principal representative of Government.He is responsible for the development of his region or District and for the efficient conduct of government business and for the maintenance of law and order." Mwisho wa kunukuu.Kanuni za Kudumu za utumishi wa umma ndio kanuni mama sisi watumishi wa umma ambazo zimemtaja RC na DC kuwa viongozi wa utendaji wa kazi serikalini katika mkoa na wilaya.
Aidha, Sheria ya TAwala za Mikoa Na.19 ya mwaka 1997 imemtaja pia Mkuu wa Mkoa kama msimamizi mkuu wa shughuli za maendeleo katika mkoa na mlinzi wa amani ndani ya mkoa.
Kutokana na maelezo hayo, Mkuu wa Mkoa hawezi kuvumilia watumishi wazembe, wezi, wasio waadilifu na wanaoharibu image ya serikali.
Kwa mfano Rais ametekeleza bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa 90% lakini hadi leo fedha zimekaa tu bila kutumiwa.Je, katika hali kama hiyo utasema Rais mbaya?
Je, tunataka Rais aende kila mkoa kushughulika na watumishi wazembe wanaodai vikokotoo wakati hawatekelezi majukumu yao?
Tunamlaumu Rais kwa uhuni wa watumishi wa aina hii ambao hawajielewi, mnataka Rais ambaye anahangaika na shida za wananchi walioathiriwa na maafa ahangaike na mambo madogo madogo ya wananchi kunyima hati miliki za ardhi.
Mimi nampongeza sana RC Makonda, RC Chalamila na yule RC wa Tabora, pale wanatimiza majukumu yao, marehemu Lowassa aliwahi kumwambia Luteni mstaafu Yussuph Makamba wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salam kuwa kiongozi lazima awe na mkali kama Simba na awe mpole kama paka.Unakuwa mkali kama Simba kama mambo hayaendi, unakuwa mpole kama mambo yanakwenda.
Arusha kuna uhuni na upigaji mwingi, haya mambo yule mpuuzi Lema alikuwa akiyanyamazia kwa sababu alikuwa akinufaika na upigaji, sikushangaa juzi kumsikia akitangaza kuwa hatogombea nafasi ya uenyekiti kanda ya kaskazini, anajua wale wanaume wawili Makonda na Gambo ni habari nyingine.
Viongozi mliopewa dhamana ya kuongoza mkoa, RC Makonda ameuwasha moto huko sio wa kawaida, watu wanatafutana huko Arusha, haiwezekani Rais leo yuko korea anatafuta hela, zinapatikana halafu wajanja wanakula, au hela zinakaa benki hazina matumizi zinavuka mwaka.
Rais Samia anaendelea na kazi na watendaji wake wanaendelea kupiga spana.Shida ukisema useme ukweli unaambiwa wewe chawa, unaambiwa wewe unatafuta cheo.Nitaendelea kutoa maoni yangu bila kujali kashfa na matusi, kwa sababu natimiza wajibu wangu kikatiba wa kutoa maoni yangu.